KLABU ya soka ya Yanga
imemtangaza aliyekuwa kocha wao msaidizi Juma Mwambuzi kuwa kaimu kocha wa
Yanga akichukua nafasi ilioachwa na kocha Cedric Kaze.
Yanga juzi Jumapili ilifikia maamuzi ya kuvunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa na kocha Cedric Kaze, kutokana na mwenendo mbaya wa timu, ambapo kati ya michezo sita iliyopita ya Ligi Kuu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee.
Mpaka anaonyeshwa mlango wa
kutokea juzi usiku, Kaze alikuwa ameiongoza Yanga kwenye jumla ya michezo 25,
akishinda michezo 16, amefungwa michezo miwili na kutoa sare mechi saba.
Akizungumzia maamuzi hayo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla amesema: “Tunategemea mwalimu Mwambusi ataichukua timu wakati tunatafuta mwalimu mkuu.
"Bahati nzuri yeye aliondoka vizuri, amepata matibabu klabu imemsaidia kwenye matibabu yake amepata nafuu. Hana ugeni wa timu tulikuwa nae kwenye Mapinduzi Cup kwa hiyo kurudi kwake sio jambo geni.
“Mwalimu mwingine tutaendelea na
taratibu nyingine za kawaida, makocha watatuma CV zao zitakwenda kamati ya
ufundi watazipitia na kuona yupi anafaa kwenye klabu yetu kwa sasa.”







Huyu ndo atafukuzwa mapema sana
ReplyDeletehivi si ni yule alikuwa Mbeya City na inaboronga?
ReplyDeleteHata hivyo Yanga hupenda janja janja hapo wanamtumia wakati wakitafuta kocha...baadaye wanamtema au kumshusha awe msaidizi
Utopolooo wanataka mtoto azaliwe leo aanze kukimbia kitu ambacho haliwezekani, kaeni jengeni team
ReplyDeleteKwani nani kakuomba utupe maoni yako?
DeleteKuelewa ni kazini sana mwambusi amekaimu na hajatangazwa kuwa kocha mkuu
ReplyDelete