BERNARD Morrison nyota wa Simba amezua utata kutokana na habari kuelezwa kuwa amekuwa na ugomvi na kocha Didier Gomes jambo ambalo limepingwa vikali na uongozi wa Simba.
Morrison ambaye alijiunga na Simba akitokea Klabu ya Yanga amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza chini ya Gomes licha ya kucheza kwenye baadhi ya mechi ambazo amesimamia kocha huyo.
Habari kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa zikieleza kwamba Morrison alikuwa na mgogoro na Gomes jambo ambalo lilimfanya asimtumie kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa.
Mchezo huo ulipokamilika dakika 90, ubao ulisoma Simba 3-0 JKT Tanzania na kuifanya Simba kusepa mazima na pointi tatu huku JKT Tanzania ikiambulia patupu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna ukweli unaozungumzwa kwamba Morrison amegomabana na Gomes hivyo huo ni uzushi na unapaswa kupuuziwa.
"Tetesi za kusema mchezaji kagombana na kocha? Tetesi ni stori za usajili, kwa nini tukae kimya kwenye stori za uchochezi klabuni? .
Sekeseka hilo limemuibua Manara ambaye ameweka wazi kwamba hatakaa kimya ikiwa kutakuwa na habari za uchochezi kuhusu Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment