MATOKEO mabovu ya timu yake ya Kagera Sugar kwenye mechi tano mfululizo yamewafanya viongozi wa Kagera Sugar kumchimbisha kocha wao ambaye alikuwa ndani ya kikosi hicho msimu uliopita.
Licha ya kuchimbishwa kwenye majukumu yake Mecky Maxime alipata muda wa kuzungumza na wachezaji wake.
Kwenye mechi tano za mwisho kabla ya kufungashiwa virago alilazimisha sare mbili ilikuwa Kagera Sugar 1-1 Gwambina, ilichezwa Uwanja wa Kaitaba na Yanga 3-3 Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa.
Nyingine ilikuwa KMC 3-0 Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru, Kagera Sugar 1-2 Azam FC na mechi yake ya mwisho kukaa benchi ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-1 Namungo FC.
Ndani ya dakika 450 wakati akisaka pointi 15 aliambulia pointi mbili kwenye sare mbili huku mechi tatu ambazo ni pointi tisa akiyeyusha zote mazima kwa wapinzani wake.
Habari kutoka ndani ya Kagera Sugar zinaeleza kuwa baada ya kupewa taarifa za kusitisha mkataba wake alipata muda wa kuzungumza na wachezaji wake ambao walikuwa wakisikitika kwa kile ambacho kimetokea.
"Hakukuwa na namna ila alipata muda wa kuzungumza na wachezaji wake ili kuwaaga hivyo ni huzuni kwa wachezaji lakini imeshatokea hakuna namna," ilieleza taarifa hiyo.
AENDE KWA WATANI ZETU MANA KWA SASA HAWANA KOCHA
ReplyDelete