March 7, 2021


 BAADA ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kugawana pointi mojamoja na Al Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi, leo Machi 7 kinatarajia kutua ardhi ya Tanzania.


Tayari kikosi hicho kimeanza safari kutoka Sudan na leo kimewasili salama nchini Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kuibukia Dar.

Saa 4:30 asubuhi kinatarajia kuanza safari ya kurudi Tanzania ili kuendelea na maandalizi ya mechi zake zijazo.

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zao zilizobaki ili kuweza kufikia malengo.

"Makosa kwenye mechi zetu ambazo zimepita tunayachukua na kuyafanyia kazi kwani kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi ndani ya uwanja," .

Simba ikiwa inaongoza kundi A na pointi zake saba, mambo yanaonekana kuwa ni mazito kwa kuwa kwa sasa timu zote zina nafasi ya kusonga mbele na kutinga hatua ya robo fainali.

Al Ahly na AS Vita baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 wanafikisha jumla ya pointi nne huku Al Merrikh nayo inakuwa na pointi moja.

Hivyo ikiwa Simba itashindwa kupata matokeo kwenye mechi zake mbili nafasiya kuangukia nafasi ya tatu ni kubwa hivyo ni lazima ijipange ili kuweza kufikia malengo. 

6 COMMENTS:

  1. Siyo siri, inabidi tumalize mchezo mapema kwa Wasudan, kwani AS VITA wanaonekana kuwa na uwezo wa kupata matokeo popote pale, hivyo game ya marudiano itakuwa ngumu sana kwetu, hawatakubali kitahisi kupigwa nje ndani na Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata simba siyo dhaifu tinavyofikiria tatizo nikwamba tumewazoe tupo nao bongo tunawaona kika siku

      Delete
  2. Kwani hao wengine wameshapata hizo point

    ReplyDelete
  3. Mnyama lazima akaze kiukweli tusipokuwa Malini hatutavuka kundi na lengo zuri heri tuongoze kundi tumkwepe mamelodi Sundowns maana tukishika nafasi ya pili sidhani Kama tuna kiwango Cha kushindana na mamelodi wako vzr wana kiwango Cha Hali ya juu Sana kwasasa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ninkuunga mkono blaza. Mechi inayokuja kati yetu na Wasudan lazima tuwapige vinginevyo tutaishia njiani

      Delete
  4. Mungu mkubwa tutavuka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic