March 8, 2021


ISMAIL Aden Rage, Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba amesema kuwa ikiwa madai ambayo yanaelezwa kuhusu wachezaji wa Al Merrikh kucheza wakiwa wamefungiwa kucheza mechi kwa miezi sita basi wana kazi ya kufuatilia kwa ukaribu madai hayo.

Kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Machi 6, Uwanja wa Al Hilal, dakika 90 zilikamilika kwa Al Merrikh kutoshana nguvu bila kufungana na kugawana pointi mojamoja.

Habari zimeeleza kuwa kuna uwezekano wa Simba kuweza kupewa pointi za mezani ikiwa itabainika ni kweli wachezaji hao walicheza wakiwa na adhabu hiyo.  

Imeelezwa kuwa Al Merrikh iliwajumuisha mchezoni wachezaji watatu waliokuwa wamefungiwa kucheza soka kwa miezi sita kutokana na kosa la kusaini mikataba kwenye timu mbili tofauti ambazo ni Al Merrikh na Al Hilal zote za Sudan.

Wachezaji hao ni Mohamed AlRashed, Ramadan Agab na Baljit khamis. Ikiwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Dider Gomes itapewa pointi hizo tatu za mezani itafikisha jumla ya pointi 9 na itakuwa inaongoza ligi.

Rage amesema kuwa Klabu ya Simba inapaswa kuwa ili timu hiyo iweze kupata pointi tatu ni lazima ifuatilie kwa umakini suala hilo kuanzia vibali vya wachezaji pamoja na mikataba yao.

"Inabidi Simba wafuatilie kwa umakini ikiwa wachezaji hao wana leseni za kucheza mechi za kimataifa kama ambavyo inaelezwa na hilo linaweza kuwapa mwanga wa kile wanachopaswa kukifanya.

"Ikiwa watajua kuhusu leseni pia wanapaswa wafuatilie kuhusu kujua kwamba wachezaji hao wanaweza kuwa wamesajili kuchezwa kwenye mechi za kimataifa za Caf na majina yao kama yapo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanapaswa kucheza mechi za kimataifa," .

4 COMMENTS:

  1. Huo ni muongozo kwani kosa kama hilo lingefanywa na Simba Al Marikh siku hiyo hiyo wangeshafika kila mahala pamoja na FIFA. Mama Barbara na kaka Manara kazi hiyo msilale Mpaka haki ipatikane

    ReplyDelete
  2. Ningewashauri Simba badala kutaka pointi za mezani wajipange kwa pointi za jasho lao. Unahangaikia pointi mbili wakati kwa 75% unajiona hatua za makundi umshavuka. Tangu lini miaka ya hivi karibuni Simba ikatamani ushindi wa mezani? Kazi hiyo ina wenyewe na mnawafahamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni issue za taratibu za soka kufuatwa usipofuata kazima kanuni za soka zifanye Kaze

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic