April 23, 2021


 KIKOSI cha Arsenal ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta leo kinatarajia kuwakosa nyota wake wawili tegemeo kutokana na sababu mbalimbali.

Mchezo wa leo ambao ni wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Emirates kwa wababe hao kusaka pointi tatu.

Pierre Aubameyang ambaye ni nahodha huyu anasumbuliwa na Malaria hivyo bado hajawa fiti kwa ajili ya kuendelea kuipambania timu yake licha ya kwamba anaendelea vizuri.

Auba alipata Malaria wakati alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Gabon.

Mwingine ni Alexandre Lacazette mwenye mabao sita ambaye aliumia nyama za paja na huenda akaukosa pia mchezo ujao dhidi ya Villarreal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic