April 12, 2021


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa lawama zote za timu yake kupoteza mchezo wowote ule ndani ya ligi zimfikie yeye kwa kuwa ni mpangaji mipango namba moja na anajua pale ambapo wanakosea.

 

Juzi, Coastal Union ilikubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Gwambina FC ambapo mabao yalifungwa na Meshack Abraham dk 9,Paul Nonga dk 31, Rajab Athuman dk 37 na Jimson Steven dk 75 na uwanja huo ulikuwa na maji kutokana na mvua ambazo zinanyesha kwa sasa.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgunda alisema kuwa lawama zote kuhusu kupoteza mchezo wake ndani ya ligi apewe yeye na sio wachezaji.

 

“Ninasema kwamba lawama zote kuhusu kupoteza kwa mchezo nipewe mimi, wachezaji wao waacheni. Ninasema hivyo kwa sababu ninajukumu la kuwafundisha na waelewe pale ambapo wanakosea makosa tunayafanyia kazi,” alisema.

 

Kichapo kikubwa ambacho Coastal Union ilipokea ndani ya ligi kwa msimu huu ilikuwa ni pale ubao uliposoma Coastal Union 0-7 Simba, Uwanja wa Coastal Union.

 

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi 24 kibindoni ina pointi 27.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic