IKIWA ni lala salama hapo kwenye Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili hakuna ambaye anakubali kuingia uwanjani kizembe kila mmoja anapambana na hali yake.
Kimbembe
kinaanza kwa wachezaji wenyewe ambapo kwa sasa unaona kwamba wanacheza kwa
kujitoa kwa ajili ya kutafuta matokeo ndani ya uwanja.
Ukiwaweka
kando hao wachezaji pia benchi la ufundi, viongozi nao wamekuwa bega kwa bega
kutoa sapoti wakishirikiana kwenye kutimiza majukumu yao uwanjani.
Hali
hii inaleta picha nzuri kule ambako tunatarajia kwenda kutokana na kila mmoja
kuwa na kitu ambacho anakifikiria kwa sasa na anakitenda kwa wakati.
Wale
ambao wapo Ligi Daraja la Kwanza hesabu zao kwa sasa ni kuona kwamba wanaibukia
ndani ya Ligi Kuu Bara huku wale wa Ligi Daraja la pili wakiipigia hesabu Ligi
Daraja la Kwanza.
Hamna
namna ya kufanya kwa sasa kwa kuwa maisha lazima yaendelee na kwa kuwa kwenye
ushindani ni lazima uoneka. Lazima itatokea wapatikane wa
kushuka na wale wa kupanda.
Njombe
Mji nao ghafla mambo yamekuwa magumu wasipopambana watarejea Ligi Daraja la
Kwanza. Boma FC ya Mbeya tayari naona imekubali mambo yaishe inapiga hesabu za
Ligi Daraja la Pili.
Kushindwa
kwa sasa haina maana kwamba wao sio bora hapana ni hesabu tu zimewagomea
wanaweza kujipanga upya wakarudi wakaendelea na kasi yao ile walipokuwa
wanaanza msimu.
Ndugu
zetu Mwadui FC wanazidi kupambana kusaka ushindi. Imani yangu ni kwamba kwa
kasi ambayo wanakuja nayo wakati huu wangeanza nayo mapema kungekuwa na wimbo
mpya ambao wanaimba.
Kikubwa
kinachohitajika ni maandalizi makini na kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa
wakati sahihi itaongeza ushindani na kuleta matokeo mazuri.
Ila
imekuwa bahati mbaya kila wakati timu nyingi kuanza kuonyesha ushindani kwenye
mzunguko wa pili ambao ni wa lala salama jambo ambalo linawaongezea ugumu
kufanya vizuri.
Zile
ambazo zinapanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza zina kazi kubwa ya kuanza kufanya
maandalizi ili ziweze kuleta ushindani wa kweli ndani ya ligi.
Kila
kitu kinawezekana ikiwa kutakuwa na mpango makini na ukweli ni kwamba kupanda
ni rahisi na kushuka ni rahisi pia lakini ukishashuka kurudi huku juu huwa
inakuwa ngumu.
Stand
United ilikuja ikashuka na ikashuka tena pale ilipokuwa kwenye Ligi Daraja la
Kwanza. Singida United ilikuja kwa kasi ila ghafla nayo kasi imekata na sasa
hata Ligi Daraja la Kwanza nako imeshushwa.
Matukio
haya yawe darasa kwa timu ambazo zinapambana kupanda kwenye ligi nazo zinapaswa
zijue kwamba huku juu mambo sio mepesi kama ambavyo wanafikiria.
Matumaini
yangu ni kwamba kupitia matukio haya yanayoendelea wamiliki wa timu, wachezaji
pamoja na mashabiki bila kuwasahau wadau wanaona namna mambo yanavyokwenda hivyo wataongeza
umakini wakati watakapokuwa kwenye ushindani.
Tunataka
kuona timu ikipanda kwenye ligi iwe na uwezo na vigezo vya kuhimili
mikikimikiki ya huku kwani hakuna kuzubaa ni mwendo wa kukimbizana.
Ukiachana
na ligi kuu ya wanaume pia kuna ligi ya wanawake hapa pia kuna umuhimu wa
kuitazama kwa ukaribu ili kutengeneza timu makini pia kwa wanawake.
Kutokana
na ushindani uliopo hasa kwenye timu za wanawake kuna umuhimu wa wadau
kujitokeza pia kutoa sapoti kwa wanawake ili nao pia waweze kuleta ushindani.
Mambo
yamekuwa mengi na magumu huku hasa katika masuala ya uendeshaji wa timu jambo
ambalo linaumiza na kuwaliza wengi ambao wanasimamia timu zetu za Bongo.
Hawa
wanapaswa pia waboreshewe na mazingira yao katika sehemu ya kuchezea maana ni
tofauti kidogo na wanaume. Unaona namna wanaume wanavyopata tabu kupata matokeo
kwenye viwanja vilivyo vibovu na havina ubora hivyo kwa hawa izingatiwe.
Katika
hili pia iwe fundisho katika kuangalia usalama na uwepo wa wachezaji wetu kwani
wanajitoa kwa ajili ya kazi kwa kufanya mchana hata usiku ila hakuna ambaye
anawajali.
Kuna
umuhimu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutazama namna ya kuwapiga tafu
wachezaji pamoja na timu kiujumla kwani wengi hali zao bado hazijawa sawa.
Mazingira
magumu ya maandalizi yanafanya timu iweze kufungwa mabao mengi kwenye mchezo
mmoja hili jambo sio nzuri kwani tunahitaji kuona ushindani wa kweli.
Katika
hili ni muhimu kutazama namna maandalizi yalivyo pamoja na fedha ambazo
zinatumika kwenye maandalizi kamili kwa timu.
Timu
chache zina uhakika kuhusu posho na stahiki za wachezaji na hii ni mbaya kwani
mambo yakiwa hivi ushindani utazidi kupungua.
Wakati
mwingine tunashindwa kuwa na timu bora inayoshiriki kwenye ligi ya wanawake
ambayo itasaidia kupata na kuibua vipaji.
Kwa
namna mambo yanavyokwenda hii haileleti afya katika maisha ya soka na ili uweze
kuushinda mpira na kupata matokeo ndani ya Uwanja ni lazima kupambana.
Wakati
uliopo kwa sasa kwa mechi ambazo zimebaki ni timu kujipanga upya kumaliza vema
lala salama huku Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) pamoja na wadau kutazama
namna mpya ya kuendelea kutoa sapoti kwa wanawake.







0 COMMENTS:
Post a Comment