e, Abdalah Sima.
Sima mwenye umri wa miaka 19 amekuwa na msimu bora ambapo amefunga jumla ya mabao 19 kwenye mashindano yote ikiwa ni manne kwenye Europa League.
Raia huyo wa Senegal ambaye pia anacheza timu ya taifa amekuwa akihusishwa pia kujiunga na washika bunduki Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
Pia amehusishwa kujiunga na West Ham United huku Manchester United nao ikielezwa kuwa wanamfuatilia kijana huyo kwa kuwa wamebadilisha sera ya usajili na kuamua kuwekeza nguvu kubwa kwa vijana.
Sima ana uwezo wa kucheza upande wa kulia na kati ikiwa atapangwa na ana uwezo wa kutokea upande wowote katika kushambulia jambo ambalo linatajwa kuwavutia mabosi wa Old Trafford.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Slavia Prague ambaye ni kiungo, Tomas Soucek anayekipiga ndani ya West Ham amesema kuwa :"Ninaweza kusema kwamba watu wa West Ham wanamtambua kijana. Ninapenda kuona kwamba mchezaji mwingine kutoka Slavia anakuja hapa ila ni safari ndefu.
"Bado ni mchezaji kijana na anaweza kuonyesha kwamba anaweza. Wengi wanajua kuhusu yeye na naona kwamba sio jambo baya kwake," .
'
0 COMMENTS:
Post a Comment