SIXTUS Sabilo, nyota wa Namungo FC inaelezwa kuwa sababu ya dili lake la kujiunga na Klabu ya Yanga kubuma ni kuchimbishwa kwa Luc Eymael raia wa Ubelgiji aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Eymael alifutwa kazi msimu uliopita wa 2019/20 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maneno yake ya kashfa pamoja ambayo yalikuwa yanaashiria ubaguzi wa rangi.
Zama zake alikuwa anahitaji kumsainisha Sabilo ambaye wakati huo alikuwa anacheza ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Sabilo imeeleza namna hii:"Sabilo alikuwa anahitajika na Yanga ila ambaye alikuwa anamhitaji alikuwa Eymael, baada ya kufutwa kazi basi na dili lake likafutwa jumlajumla, " .
Kwa sasa Sabilo yupo ndani ya Namungo FC akiendelea kupambania mkate wake wa kila siku na timu yake inashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho ikiwa hatua ya makundi
0 COMMENTS:
Post a Comment