SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa walichokiona mbele ya Mwadui FC jana ililikuwa tofauti na walivyotarajia kwa kuwa walitarajia timu hiyo ingefunguka jambo ambalo lilikuwa tofauti.
Mabingwa hao watetezi walishinda bao 1-0 ambalo lilipachikwa kimiani na nahodha mzawa, John Bocco aliyekuwa benchi akisoma mchezo huo.
Kocha huyo ameongeza kwa kusema kuwa walijitahidi kuwasoma wapinzani hao kwa muda ili kuweza kujua namna gani wanaweza kushinda ila mambo yakawa tofauti.
"Ninashukuru Mungu kwamba tumeshinda na kupata pointi tatu mbele ya Mwadui ila ilikuwa ni kwa tabu sana kwa kuwa wapinzani wetu walikuwa imara muda wote.
"Unajua tulijaribu kuwatazama wapinzani wetu kwenye mechi zao zilizopita tukajua kwamba watafunguka kwenye mchezo wa leo ila mpango wao ukawa ni kwenye kutafuta pointi moja jambo ambalo linaonekana ilikuwa kwenye mpango wao.
"Tunachokishukuru ni kwamba ambacho tumekipata ni pointi tatu muhimu na tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo," amesema.
Simba imefikisha pointi 52 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 22 na vinara ni Yanga wenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 25.
Mbinu waliyotumia mwadui imewasaidia kupunguza magoli tu,Ila laiti uwanja ungekua umefyekwa vizuri basi mwadui angeoga magoli mengi Sana,mpira anaocheza Simba Kwa zile nyasi isingewezekana hata kidogo,hata goli la kagere kama sio nyasi kua ndefu mpira ulikua unazama nyavuni Ila pongeza Kwa mwadui wamejitahidi Sana kimbinu.
ReplyDelete