VIUNGO washambuliaji wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo na Salum Kihimbwa wamerejesha matumaini kwenye kikosi hicho baada ya kupona majeraha yao.
Nyota hao wawili walikuwa wanasumbuliwa na majeraha ya misuli waliyopata jambo lililowafanya wake nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kaimu Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Vincent Barnabas alisema kuwa nyota hao walianza mazoezi mepesi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Barnabas
alisema kurejea kwa viungo hao kutaimarisha kikosi chake katika safu ya kiungo ambayo hivi sasa inachezwa na
Baraka Majogoro na Jaffar Kibaya.
"Habari njema kwa mashabiki wa Mtibwa Sugar ni kuwa viungo wao Kihimbwa na Chanongo wiki iliyopita walianza mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya wiki ijayo kuanza kuanza mazoezi magumu.
"Viungo hao walikosekana kwa muda mrefu katika kikosi changu kutokana na majeraha hivyo ninafurahi kuwaona wakirejea uwanjani," .
0 COMMENTS:
Post a Comment