April 19, 2021


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anatambua mchezo wa kesho dhidi ya Gwambina FC utakuwa mgumu kutokana na ushindani wa ligi kuwa mkubwa.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Gwambina Complex zama za Cedric Kaze ubao ulisoma Gwambina 0-0 Yanga na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Kesho timu hizo zina kazi ya kusaka pointi tatu ili kutimiza malengo waliyojiwekea ambapo Yanga wamesema kuwa wanahitaji pointi tatu.

"Ninajua kwamba utakuwa mchezo mgumu kutokana na nafasi ambayo wapinzani wetu wapo kwa wakati huu mbali na hilo pia ni timu imara.

"Imani yetu ni kuona kwamba timu inapata matokeo chanya. Ukitazama nafasi ambayo Gwambina ipo na nafasi yetu ni miongoni mwa sababu ambazo zitaongeza ugumu kwenye mchezo huo," .

Haruna Niyonzima, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata matokeo mazuri.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ina pointi 54 inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 na pointi zao ni 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic