April 12, 2021

 


Na Saleh Ally

NAJUA nimewaudhi sana Yanga kwa kuwaambia ukweli, wako waliotukana sana na wengine wakasema kila wanalojua lakini sasa huu ndio ukweli, hakuna mjadala.

 

Juzi, Yanga imepata sare ya tisa katika mechi zake 24 za Ligi Kuu Bara, sare hizo zinaifanya Yanga kuwa moja ya timu zenye sare nyingi katika Ligi Kuu Bara.

 

Timu zenye sare nyingi ni kuanzia nane hadi kumi nakitu ndani ya michezo 24.Hii inaonyesha hivi, kama umecheza mechi 24, halafu una sare tisa, maana yake ni karibu asilimia 40 ya mechi zako ni sare, vipi unaweza kupambana kuwania ubingwa wakati una sare za kiwango hicho?

 

Timu bora lazima iwe na ushindi mara nyingi zaidi.Katika mechi 24, Yanga wameshinda 14, wanaingia katika kundi la timu zilizoshinda mechi nyingi sawa na Simba. Lakini unaona Simba wana nafasi ya kwenda kushinda mechi nyingi zaidi ya Yanga kwa kuwa wamecheza mechi 20 na wameshinda 14.

 

Kama wana mechi 20, wameshinda 14, maana yake ni zaidi ya asilimia 60 niushindi. Wana sare nne na wamepoteza mbili na hadiwanawafikia Yanga kwa idadi ya mechi za kufunga, bila shaka watakuwa wameongeza mechi za ushindi.

 

Yanga mwendo wao katika ligi kuu ni mzuri wawastani na hii wastani imezalishwa katika mzunguko wa pili baada ya kikosi chao kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza ambao kilimaliza bila ya kufungwa.

 

Tokea Yanga iingie katika mzunguko wa pili, imefanikiwa kushinda mechi moja tu katika saba, wamepoteza moja na hii ni sare ya tano. 

Huu si mwendo mzuri hata kidogo na vigumu kusema wamekaa vizuri kuwania ubingwa.

 

Yanga na hasa mashabiki hawataki kusikia neno kwamba “wamekaavibaya”, “timu yao bado haijatulia”, “timu yao inataka kuimarishwa” nakadhalika, wangependa kusifiwa zaidi lakini huu ndio ukweli.

 

Nina bahati kwa kuwa nilianza kusema mapema sana licha ya kuonekana kama ninawasakama, kwa wale waliona tabia ya kukubali ukweli, watakuwa wanaona na hata kama ni kimyakimya, wanaamini au kukubali nilichosema.

 

Yanga bado hawana timu mbaya lakini wakubali, presha ya Simba inawafanya wakati mwingine watoke relini nakufanya mambo ambayo hayawahusu au si wakati mwafaka kuyafanya.

 

Kingine, kumekuwa na haraka kubwa na hasa kwa kuwa kumaliza mzunguko wa kwanza bila ya kupoteza mchezo kuliwafanya waamini kuwa wako vizuri.

 

 

 

Uhalisia ni hivi, pia nilisema mapema. Kwa kuwa ligi imesimama, Yanga itakuwa moja ya timu zilizoathirika kwa kuwa ndio itakuwa inaanza kutengeneza mwendo upya.

 

Sare nilitegemea kwamba ingewezekana lakini mechi dhidi ya KMC, Yanga wangeweza hata kupoteza na KMC walikuwa bora zaidi. Hii maana yake, lazima warudi wakarekebishe makosa yao na kujikumbusha kwamba hakuna timu inayoweza kuwania ubingwa katika ligi kwa kuwa na sare katika mechi zake kwa takriban asilimia 50.

 

Bado ninakumbusha, kuanzia hiyo juzi, siku 30 za Yanga zitakuwa ngumu kwa kuwa sasa wanafuatia Biashara United, halafuGwambina, watafuatia Azam FC halafu Simba.

 Ni lazima kuwe na utulivu badala ya kuanza kulaumiana na kuvurugana, mwisho itakuwashida. Kama watatulia, nafasi ya kurekebisha mambo na kurudi wanayo.

 

 


7 COMMENTS:

  1. Umechapa kwenye mshono wa chura na nyani

    ReplyDelete
  2. Nani ajuaye kesho yake?

    ReplyDelete
  3. Sare tisa ni sawa na kupoteza points 18 ambazo ni sawa na kufungwa mechi 6

    ReplyDelete
  4. Kutokana na uliyoyasema, sasa tegemea Tanga mupeleka mashtaka ama TFF au Fifa

    ReplyDelete
  5. YANGA HAIWEZI KUWA BINGWA WALA NAFASI YA PILI HAWAPATI WATAISHIA NAFASI YA NNE AU TANO.

    ReplyDelete
  6. Ijapokuwa hawataki kuambiwa kuaandaa timu lakini huu ndo ukweli mchungu wapende wasipende hata kama hawataki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic