NAHODHA wa kikosi cha Arsenal, Pierre Aubameyang, kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta amesema kuwa sababu kubwa ya kutokuwa kwenye ubora wake ni kuumwa jambo ambalo lilimfanya apungue kilo kadhaa.
Arsenal imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua ndani ya uwanja na imeshindwa kutinga hatua ya fainali ya Europa League baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wao walipocheza na Villarreal inayonolewa na Unai Emery.
Emery ambaye aliwahi kuifundisha timu hiyo na kufutwa kazi alikiongoza kikosi chake kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 na ule wa pili ubao ulisoma Arsenal 0-0 Villarreal.
Auba raia wa Gabon mwenye miaka 31 amesema kuwa anaweza kubeba lawama kwa timu yake kushindwa kufanya vizuri kwa sababu hajatimiza majukumu yake kwa kuwa anacheza chini ya kiwango.
"Wanaonikosoa naumia lakini lazima nikubali kwa kuwa nimecheza chini ya kiwango. Baada ya kuugua Malaria nilipungua kilo kadhaa na hata ubora ukawa chini,".
0 COMMENTS:
Post a Comment