HASSAN Salum, Kocha Msaidizi wa Gwambina FC amesema timu yake haitatoa mapumziko kwa wachezaji wake katika kipindi hiki cha kupisha mashindano ya kombe la Azam Federation Cup.
Kocha huyo amesema kuwa kwa sasa wataendelea na mazoezi ya kujiandaa na michezo minne mfululizo ambayo wamepangiwa kucheza ugenini.
Salum amesema :-“Kwa sasa ligi ipo ukingoni na sisi kiukweli tuna ratiba ngumu ambapo tutacheza michezo minne ugenini ligi ikirejea hivyo hatutatoa mapumziko yoyote kwa wachezaji badala yake tutaendelea kujiandaa.
“Ratiba inaonyesha kwamba tutacheza na Namungo FC, Mbeya City,Tanzania Prison pamoja na Azam FC kiukweli ni michezo mizito na michezo ya maamuzi kwa hatma ya klabu yetu hivyo tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba tunakuwa na timu bora ya kushinda michezo hiyo,” amesema.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Gwambina FC ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 29.
0 COMMENTS:
Post a Comment