SAFARI imeanza kuzidi kupamba moto ya kumsaka mshindi wa taji la Azam Sports Federation baada ya droo ya robo fainali kuchezwa na kila timu kujua nani atakutana naye.
Labda watani wa jadi wanaweza kukutana fainali ikiwa kila
mmoja atapambana kwa jitihda zake na kuweza kushuhudia ile ladha ya Kariakoo
Dabi nyingine baada ya ile ya awali kwenye ligi iliyopangwa kuchezwa Mei 8,
2021 kuyeyuka na inatarajiwa kuchezwa Julai 3.
Hapa Spoti Xtra inakuletea hatua kwa hatua namna timu hizo
zilizotinga robo fainali pamoja na wapinzani wake walivyofika hapo walipo,
twende sawa:-
Simba v Dodoma Jiji
Huku kurasa zilifunguliwa
Dodoma Jiji ilishinda mbele ya Kipigwe FC jumla ya mabao 7-0
Uwanja wa Jamhuri, Dodoma hatua ya 32 bora na hatua ya 16 bora ilishinda mbele
ya KMC kwa mabao 2-0, ilikuwa Mei Mosi.
Rhino Rangers v Azam FC
Rhino Rangers v Azam FC, Rhino Rangers timu pekee iliyotinga hatua ya robo fainali ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza itakutana na Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Walianzia huku
Hatua ya 16 bora, Rhino Rangers ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Arusha FC.
Azam FC Februari 27 ilishinda bao 1-0 mbele ya Mbuni FC
inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Uwanja wa Azam Complex. Azam FC ilikuwa
nyumbani hatua ya 16 bora Azam FC ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania.
Biashara United v Namungo FC
Hizi zote zinashiriki Ligi Kuu Bara ambapo mchezo wao tayari umeshakamilika ilikuwa ni Uwanja wa Karume, Mara. Mshindi wa mchezo huu atakutana
hatua ya nusu fainali kati ya mshindi wa mchezo wa Mwadui FC dhidi ya Yanga.
Mwendo wao
Namungo FC iliibuka na ushindi mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Majaliwa kwa bao 1-0. Hatua ya 16 bora Namungo ilishinda mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mwadui FC v Yanga
Timu zote mbili zinashiriki Ligi Kuu Bara ambapo Mwadui FC inakumbuka kwamba ilipokutana na Yanga zama zile ikinolewa na Khalid Adam huku Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze, ubao wa Kambarage, Shinyanga ulisoma Mwadui 0-5 Yanga.
Mshindi wa mchezo huu atakutana na mshindi wa mchez kati ya
Biashara United v Namungo FC kwenye mchezo wa nusu fainali.
Safari zao sasa
Mwadui FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Salhina Mjengwa hatua
ya 32 bora ilishinda mabao 4-1 mbele ya Gwambina FC, Uwanja wa Mwadui Complex.
Ilikuwa ni Februari 26.
16 bora, Aprili 30, Mwadui FC ilishinda mabao 2-0 dhidi ya
Coastal Union, Uwanja wa Mwadui Complex.
Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold, Uwanja wa Uhuru
ilikuwa ni Februari 27.
ilitinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela, Aprili 30.
Hat trick zipo
Anuary Jabiry wa Dodoma Jiji alisepa na mpira wake wakati
timu hiyo ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Kipigwe alifunda dakika ya 20,35 na 68.
Relliats Lusajo wa Namungo alitupia mabao matatu na kusepa
na mpira wake ilikuwa dakika ya 23,26 na 41.
0 COMMENTS:
Post a Comment