May 24, 2021


IMEELEZWA kuwa nyota nane wa Yanga kwa sasa wana uhakika wa kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2021/22 huku wengine wakisubiri ripoti ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Miongoni mwa nyota ambao mpaka sasa hawajui hatma yao na wana asilimia kubwa ya kusepa ndani ya kikosi hicho ni pamoja na mshambuliaji Fiston Abdulazack ambaye mkataba wake msimu ukiisha naye mkataba wake unameguka.

Hana uhakika wa kubaki Yanga kwa kuwa hajaitwa kuzungumza na mabosi wake na kipengele cha kuongeza mkataba wake inaeleza kuwa kilikuwa kinaeleza kuwa itategemea na uwezo wake ambao atauonyesha ila mpaka sasa amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza.

Taarifa zimeeleza kuwa nyota ambao wana uhakika wa kubaki ndani ya Yanga kwa msimu ujao ni wale ambao walikuwa wanaanza kikosi cha kwanza katika mechi tatu zilizopita chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ni pamoja na:-Saido Ntibanzokiza, Yacouba Songne, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Kibwana Shomari, Dickson Job, Feisal Salum, Abdalah Shaibu, 'Ninja'.

Kuhusu suala hilo, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha.

"Jukumu la usajili ni la kocha, katika hilo kuelekea msimu ujao kila kitu tumemuachia yeye, hivyo ndiyo sababu ya kumuwahisha kuja kumaliza msimu kwa kuangalia wachezaji wengi," alisema.

Chanzo: Spoti Xtra

8 COMMENTS:

  1. Wewe hii story ndiyo unatumika kudemolize Yanga kwanini usiandike hayo kuhusu Simba ,mmekuwa mnatumka kurubuni Wachezaji wetu ,halafu mnasifia Simba ulivyo nzuri huku mnacheza Mpira wa Bar

    ReplyDelete
  2. Usajilii etii ambundo hhhh yangaaa mtaaishia round yaa awali

    ReplyDelete
  3. Washauriwe kusajili kikosi kamili kama walivofanya msimu huu kwasababu vichaka vipya na komba wapya waweze kuwalea wenyewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic