AGREY Morris, nahodha wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa kwa sasa hawana presha ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara na badala yake watapambana kupata matokea katika mechi zao ambazo zimebaki.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ipo nafasi ya tatu na ina pointi 60 zilizotokana na mechi 30.
Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ni vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25, watani zao wa jadi Yanga wapo nafasi ya pili na pointi 61 baada ya kucheza mechi 29.
Nahodha wa Azam FC, Agrey Morris, amesema: “Bado tunapambana ila hatuna presha na ubingwa kwa sababu ili upate ubingwa lazima ushinde hicho ndicho ambacho tunahitaji kukifanya.
"Nafasi ambayo tupo sio mbaya kwa sababu tupo sehemu nzuri na hilo kwetu ni furaha. Kazi bado inaendelea na tutapambana kupata ushindi katika mechi zetu.”
Leo kikosi cha Azam FC kimekwea pipa kuwafuata Rhino Rangers kwa ajili ya mchezo wa wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Mei 26, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Azam ina akili zake tamam na wakuheshimika imeshatambuwa kwa hali ilivo ubingwa 95% na kama si 100% ni wa Simba
ReplyDelete