May 9, 2021


Anaandika Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba:-

 Samahani!!


Ni neno moja lenye maana sana kwa muungwana.

Kuanzia Jumatatu hii nilizunguka kwenye vituo vya redio,televisheni na magazeti kufanya promotion kubwa kuelekea mchezo wa jana ambao ulikuja kuhairishwa baadae.

Sijilaumu kwa kile nilichofanya kwa niaba ya klabu yangu, lakini nimeumizwa sana kuona mashabiki wake hawakupata walichokitarajia.

Najihisi ni mkosaji na nadhani kuna haja ya kuwajibika kwa kitendo kile, nilitumia nguvu kubwa kuhakikisha tunajaza uwanja, lakini matokeo yake ni maumivu yaliyoacha doa kuu.

Nawaza kwa hisia, kwa nini sauti yangu iwe sehemu ya kuwapa maumivu wengine? Wangapi wamejeruhiwa kimwili ná kiaikili kwa kilichotokea jana?

Naogopa na naomba msamaha sana kwa mashabiki wote hususani mliokuja jana kwa Mkapa. Binafsi nipo katika kipindi kigumu mno. Kila nikiwafikiria mashabiki wale ambao always, ndio huufanya mchezo huu wa soka kuwa hivi ulivyo sasa.

Inawezekana nisiwe nahusika hata kidogo kuhairishwa kwa mchezo ule, but, (lakini) nitakuwa mpuuzi nisiposema samahani kwenu, imani yangu taarifa rasmi ya klabu juu ya kadhia hii nzito itatolewa.

Mungu awabariki sana ndugu zangu.

7 COMMENTS:

  1. Makenge yadiyojua utu yamewaumiza sana wapenda mpira, nina hakika mahudhurio yatashuka sana.

    ReplyDelete
  2. Iftar imefanya kazi, acheni kuzuga

    ReplyDelete
  3. Ni jambo baya sana kutesa maelfu ya mashabiki kiasi kill. Watu wamesafiri kutoka nje na ndani ya nchi, wameingia uwanjani wengine kutoka saa 3 asubuhi, wamefunga ramadhani, halafu Wizara na TFF mnakuja haribu ratiba? Kabla ya kubadili ratiba kwanini hamkuitisha kikao cha dharura cha pande zote husika-Wizara ya Michele,TFF,YANGA,SIMBA,Chama cha Waamuzi,Bodi ya Mashindano, Kamati ya Ulinzi na Usalama, nk mkajadili kwa pamoja na kukubaliana kwa pamoja. Kwanini hekima hiyo haikutumika?

    ReplyDelete
  4. Ni jambo baya sana kutesa maelfu ya mashabiki kiasi kill. Watu wamesafiri kutoka nje na ndani ya nchi, wameingia uwanjani wengine kutoka saa 3 asubuhi, wamefunga ramadhani, halafu Wizara na TFF mnakuja haribu ratiba? Kabla ya kubadili ratiba kwanini hamkuitisha kikao cha dharura cha pande zote husika-Wizara ya Michezo,TFF,YANGA,SIMBA,Chama cha Waamuzi,Bodi ya Mashindano, Kamati ya Ulinzi na Usalama, nk mkajadili kwa pamoja na kukubaliana kwa pamoja. Kwanini hekima hiyo haikutumika?

    ReplyDelete
  5. Safari mi starehe dogo jiongeze

    ReplyDelete
  6. Mwenye blog usijifanye mhariri na kulihusu kitu kinachoendana na fikra zako kirushwe by shortly mbumbu juzi mlipelekwa Semina NIMEMALIZA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic