May 23, 2021


NYOTA wa kikosi cha klabu ya Kaizer Chiefs wameweka rekodi ya kipekee katika dimba la Mkapa, Dar es Salaam baada ya kufanikiwa kucheza mbele ya mashabiki baada ya kupita mwaka mzima na miezi miwili tangu mara ya mwisho wafanye hivyo.

Kaizer jana walikuwa na kibarua kizito cha mchezo wa marudiano robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa FNB ‘Soccer City’ nchini Afrika Kusini.

Tangu mwezi Machi mwaka jana, nchini Afrika Kusini imezuia kuingia kwa mashabiki viwanjani kama sehehu ya kuweka tahadhari ya kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Akizungumzia hali hiyo kocha mkuu wa Kaizer Chiefs, Gavin Hunt amesema: “Shirikisho la soka la Afrika Kusini lilizuia uwepo wa mashabiki uwanjani tangu mwezi Machi mwaka jana, na tangu hapo wachezaji wangu hawajapata nafasi ya kucheza mbele ya mashabiki.

“Hivyo wachezaji walikuwa wanausubiria mchezo huu kwa hamu kubwa kuipata tena ile hisia ya burudani ya mashabiki uwanjani, kama ilivyo kwa nchi za Ulaya ambapo mashabiki wameanza kurejea viwanjani.”

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic