May 10, 2021




 MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Coastal Union dhidi ya Simba umeahirishwa kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB).

Taarifa hiyo imeeleza namna hii:"Mchezo wa VPL na.259, (Simba vs Coastal Union) uliopangwa kuchezwa Mei 11,2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, umeahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine kwa sababu Simba inalazimika kusafiri siku hiyo kwenda A.Kusini kwa ajili ya mchezo a CAFL dhidi ya Kaizer Chhiefs Mei 14,". 


Rekodi zinaonyesha kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilisepa na pointi tatu mazima.

Baada ya dakika 90, ubao ulisoma Coastal Union 0-7 Simba na nahodha John Bocco alisepa na mpira baada ya kufunga hat trick.

11 COMMENTS:

  1. Cinema ya baba (TFF)na mke wake (mkia) zinaendelea bila kujali

    ReplyDelete
  2. Na Ni sababu hizo hizo zilizopelekes mchezo wa tarehe 8 kufanyiwa figisufigisu hadi ikabidi kuahirishwa. Usanii wa kijinga kabisa.

    ReplyDelete
  3. Na Ni sababu hizo hizo zilizopelekes mchezo wa tarehe 8 kufanyiwa figisufigisu hadi ikabidi kuahirishwa. Usanii wa kijinga kabisa.

    ReplyDelete
  4. Huwezi amini wanaenda AKusini huku Wana viporo Sasa tunazidi kupata ukweli hili jamaaa linaitwa KARIA sijui Kacheka je linaweza kutujibu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi bado Yanga wana matumaini ya kuwa mabingwa? Naona wanalalamikia viporo vya Simba, kwani Yanga akishinda mechi zake viporo vya Simba vitafaa tena? Acheni ujinga, chezeni mpira. Au na hili la viporo mnalitafutia kanuni?

      Delete
  5. TUWAOMBEENI TFF, MAANA WANAKOELEKEA NI KUBEBA MIKIA MPAKA AIBU.
    AU NA HII ILIKUA MAAGIZO KUTOKA WIZARANI. BADO MIKIA NA NAMUNGO HAWAJACHEZA HATA MECHI MOJA.
    RATIBA INAPINDULIWA NDANI YA MASAA, KWELI SOKA IMEVAMIWA

    ReplyDelete
  6. Watu aina hiyo kisha wanawafungia kina Mwaka... na wao wajiuzulu tu ili kuondoa ombwe lililopo TFF

    ReplyDelete
  7. Kama simba ataingia fainali caf ligi haitaisha maana timu zingine zitakuwa zimemaliza mechi simba bado ratiba ya ligi ni mbovu sana.Mbona hao wengine wanaocheza caf na wapo robo fainali ligi zao zipo fresh

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic