May 23, 2021

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba, Bernard Morrison amefunguka kuwa ana imani kubwa klabu yake itaendelea kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka 15 hadi 20 ijayo.

Nyota huyo mwenye uraia wa Ghana alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho jana kiliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini, katika robo fainali ya pili ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Licha ya ushindi huo Simba ilishindwa kusonga mbele kutokana na tofauti ya bao moja baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Afrika Kusini.

Baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo Morrison amesema: “Ninajivunia sana kuvaa jezi hii ya Simba, tumetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini tunajipanga kuhakikisha tunashinda makombe yote yaliyobaki. Simba itaiwakilisha Tanzania kwa miaka 15 Hadi 20 ijayo,"


12 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Mtu akisema kweli anavuta bangi? Hana akili? Kati ya Morrison na Wale wapumbavu wanaoshabikia timu za mataifa ya kigeni zinapokuja kucheza na timu zetu nani mgonjwa wa akili?

      Delete
    2. Kidimbwini fc🤣🤣

      Delete
  2. Morrison wacha kuwapa Kihoro matopolo usije kuwamaliza kwa already watete sana wanaifikiri hiyo siku ya siku

    ReplyDelete
  3. Wataanguka muanguko wa mende aliepuliziwa dawa

    ReplyDelete
  4. huyu morison ana matatizo ya akili na haihitaji utaalamu kumuelewa bali mtizame usoni tu utajua na akiongea ndio kabisaaaa

    ReplyDelete
  5. Yanga inaatuambiaaa inaatengenezaa timuu tyr kimataifaa timuu nne wasijeeesemaaa hawaajuii kilichookuaa kinaaendeleaa

    ReplyDelete
  6. Utopolo ni baiskeli ya kunna visu.Kelele nyingi lakini haiendi popote.Ipo pale pale.Na visingizio vipya kila msimu.

    ReplyDelete
  7. Ati leo ndio wanasema mgonjwa wa akili lakini alipojiunga Simba mlimpandisha Mpaka mawinguni na alipkukataeni sasa munasema mwendawazimu sasa mtaziona ghadhabu zake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic