May 25, 2021


 ITAKUWA ni mwendo wa mchakamchaka leo, Uwanja wa Kambarage pale Mwadui FC itakapokutana na Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali kutokana na timu zote mbili kulipigia hesabu kombe hilo.

Leo Mei 25, Mwadui  ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza itawakaribisha Yanga, Uwanja wa Kambarage kwa timu hizo kusaka ushindi  ndani ya dakika 90.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Mwadui FC, David Chakala amesema kuwa vijana wapo tayari kwa ajili ya kuwakimbiza wapinzani wao ndani ya dakika 90.


“Mwendo wa mchakamchaka kwa kuwa vijana wana morali kubwa na wanahitaji ushindi hivyo baada ya dakika 90 mashabiki wetu watajua nini ambacho tumekipata ila ukweli ni kwamba tunahitaji ushindi,”.


Kwa upande wa Yanga, Kocha wa Makipa, Razack Siwa amesema kuwa wachezaji wapo tayari na watapambana kupata matokeo katika mechi zao.


“Ukweli ni kwamba tunahitaji kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho na wachezaji wapo tayari hivyo kikubwa ni kwamba tunahitaji ushindi,” amesema Siwa.


Mwadui ilitinga hatua hiyo kwa kuifunga Coastal Union mabao 2-0 huku Yanga ikitinga hatua hiyi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.


Mshindi wa mchezo huo anatarajiwa kutinga hatua ya nusu fainali na atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara na Namungo ambaye ni Biashara United.

Biashara United ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo kwenye mchezo wa robo fainali, Uwanja wa Karume, Mara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic