SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Azam TV Limited kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10.
Makubaliano hayo ambayo wameingia nao yana thamani ya Shilingi bilioni 225.6.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na viongozi waalikwa waliokuwa katika hafla hiyo ya kutia saini mkataba wa Haki za Television, (Tv Rights) katika Hotel ya Hyat iliyo Posta, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema:"Nachukua fursa hii kuwapongeza Azam Media Limetide chini ya Mkurugenzi wao Tido Muhando kwa kufanikiwa kushinda tena zabuni hii hivyo kufanya kazi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania, chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuendesha ligi hii," .
Pongezi sana. Ila naona miaka kumi ni mingi mno kwamba baada ya miaka mitano tutakuja kuona mkataba ulioingiwa ni mdogo mno. Sina uhakika kama TFF na Bodi ya ligi wamejifunza haya kwa nchi zenye uwekezaji afrik au hata Ulaya. Inawezekana pia Azam Media wamefanya hivi kuhofia chombo kingine kuchukua nafasi hiyo na kikiwa na mkataba mnono zaidi.
ReplyDeleteKila mfanya biashara hulenga kuongeza faida. Hivo, TFF wangelitazama Hilo. Umeona udhamini was sport pesa kwa Simba sc ulivopimwa. Wakati unaingiwa, ulikuwa bora kwa mazingira hayo.
ReplyDeleteHiyo figure ukiigawanya kwa mwaka uraona kama 22.5. je thamani hiyo itabaki constant kwa kipindi chote hicho bila kuathiri ongezeko la thamani?
Duuuh Miaka 10? Jamani jamani Nchi hii? Tshs 255.6 Bilioni tu. Tunapigwa
ReplyDeleteDuh mwenye nacho ataongezewa ila kwa hiyo hela ni ndogo sana lakini kwakuwa hakuna competition basi
ReplyDeleteHivi labda jamani mimi naomba mnieleweshe. Mapato ya Club yameshuka sana baada ya Ligi kuanza kuonyeshwa kwenye TV. Kodi ya Serikali bila shaka imepungua kutokana na kushuka kwa viingilio. Je kwa mazingira ya kwetu je tuendelee kuonyesha mpira? Azam wao wana deny watu wasione kwenye YouTube mpira Live. Wanataka wanunue ving'amuzi. Mtu mmoja anafaidika. Ulaya mpira unaonyeshwa na watu wanajaa viwanjani serikali inakusanya kodi. Kwa nini mpira ukichezwa DSM watu wa DSM wawe denied kuona kwenye TV ili mapato ya viingilio yapande? Hapa Tanzania asilimia 30 ya muda wa vijana unaishia kujadili Yanga vs Simba, Kwa nn serikali isidiscourage hii hali kwa kuvuna mapato? Hasara tunayopata kama Taifa ni kubwa. NI MAWAZO YANGU TU
ReplyDeleteEti Kuna watu wanasema kaboresha ,huyo ndiyo waresi Kakalia miaka 10 pesa hiyo? Bora wangeweka 5 yrs ,najua wameshikishwa tu.
ReplyDeleteNdugu zangu tunaotokea Vijijini Tena mbali kila ving'amuzi vipo Tena zaidi na huu Umeme wa REA Nchi nzima ,kwa Mkataba huu hizi ni dhama za kupewa shanga ukatoa Dhahabu.Watu Wana dhambi;
ReplyDeleteAcheni mihemko ndugu zangu. Huu mkataba ni mzuri sana na unakwenda kuleta ahueni kwa klabu zote zinazo shiriki ligi kuu ya vodacom.
ReplyDeleteWe sikiliza mihemuko kwa lipi ?tusiishi kwa mazoea mambo Kama haya ndiyo yanafanya Ligi yetu iwe ya hovyo na hatushtuki, mfano Ligi zote Duniani zilisimama tukacheza Ligi mpaka tukajisifia mpaka Leo hatujamaliza huku Ligi zote Ulaya wamemaliza,sisi huku ni Simba,Board ya Ligi na hao AZAM TV na hizo Kanuni zao za Mpira
ReplyDelete