SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeweka wazi kwa kuipandisha Tanzania kuwa kwenye nafasi ya nchi 12 zitakapoleka timu nne katika michuano ya kimataifa msimu ujao wanatoisimamia upande wa ngazi ya klabu.
Hiyo ni kufuatia Simba kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na kuwapiga bao Libya.
CAF imeipandisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 12 ambazo zinapeleka timu nne msimu ujao wa 2021/22 ambapo mbili zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na zingine Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa mujibu renki za CAF, Tanzania imepanda hadi nafasi ya 12 ikiishusha Libya iliyokuwa katika nafasi hiyo ambayo imeteremshwa kwa nafasi tatu ikiwa pointi 13.5.
Kitendo cha Simba kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, kimeifanya Tanzania kukusanya pointi 27.5.
Spoti Xtra limezungumza na Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Salum Madadi ambaye amefafanua juu ya timu ambazo zitakuwa na nafasi ya kushiriki michuano hiyo.
“Nafasi ya kupeleka timu nne namna ilivyo ni kwamba, mbili zitatoka kwenye ligi kuu kwa maana ya mshindi wa kwanza na wa pili, na zingine mbili katika Kombe la FA kwa zile ambazo zimecheza fainali.
"Lakini ikitokea bingwa wa ligi kuu ameingia fainali ya Kombe la FA, basi atakwenda kuiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa halafu mshindi wa pili wa FA atakwenda Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya hapo mshindi wa pili wa ligi atakwenda Ligi ya Mabingwa na mshindi wa tatu atacheza Shirikisho,” alisema Madadi.
KAULI YA AZAM
Mkuu wa Idara ya Habari ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka za Kazi’, amezungumzia suala hilo akisema kwa upande wao walishajiandaa mapema kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.
“Binafsi Azam, haikushangazwa juu ya suala hilo kupata nafasi nne kwa kuwa tayari tulishajiandaa mapema kushiriki michuano ya kimataifa kupitia ubingwa wa ligi kuu au Kombe la Shirikisho, hivyo hata kama hizo nafasi zisingekuwepo bado sisi malengo yangekuwa hivyo ndiyo maana tunaendelea kupambania ubingwa," .
YANGA WANASEMAJE?
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Hassan Bumbuli, amebainisha kwamba: “Kitu ambacho huenda hakifahamiki ni kwamba Yanga ipo kwenye malengo makubwa ya kucheza michuano ya kimataifa, lakini siyo kwa sababu ya hizo nafasi za upendeleo.
“Kitu pekee ambacho tunachokiamini ni kushinda ubingwa wa ligi kuu au Kombe la FA ili tuweze kupata nafasi ya uhakika, lakini siyo hiyo ambayo imekuwa ikitajwa.”
Lakini viongozi wa Yanga wanasema wao hawatoshiriki kutokana kubebwa na Simba lakini eti kwa jitihada za wenyewe. Jamani hawa watu hawana shukueani. Wangezutsja hizo juhudi zilizowapa nafasi
ReplyDeleteMtaenda kwa mbeleko Hilo lipo wazi
ReplyDeleteDaa ukibebwa bebeka basi acheni shukrani ya Punda mbona misimu kadhaa nyuma hamkua na kauli hizo leo kisa mnaona kuna uhakika wa timu nne ndio mnaanza shombo haya shukrani ya punda mateke tutaona huko mbele ndio tutajua wakimataifa nani.. all the best
ReplyDeleteViongozi wetu wa mpira ndo be chanzo Cha timu zetu kuboronga. Ukitathimini kauli za Hawa viongozi be wawili, unaliona Hilo waziwazi.
ReplyDeleteAhhh. Viongozi wetu yanga mnstutia aibu. La msingi tuanze matayarisho kama usajili na masuala ya kifedha ili na sisi tuje fanya vizuri kama simba. Basi nynyi mmebaki kuendeleza chuki. Mimi natudia tena na kwa mara ya mwisho. NITARUDISHA KADI IKIWA SERA ZA TIMU YETU YANGA NI MAJUNGU CHUKI NA FITINA. nimevjoshsa na ustaarabu wa kiisraili.
ReplyDeleteNimefurahia comments mbalimbali. Hapa ni kuwa Tanzania imepanda hadi nafasi ya 12 na inahitajika timu 4. Naona wivu sana nikiona nchi nyingine wakishiriki timu 4. Ninaamini Simba, Yanga na Azam wakifika wote fainali itapendeza sana. Tuache upumbavu wa fikira
ReplyDeleteMwenyewe amesema niombeni nikupeni na mkinishukuru nitakuongezeni lakini hawa jamaa hawajuwi kushukuru na ndio mana hawana maendeleo na hakuna wakuwafundisha
ReplyDeleteoyaa sio wote mashabiki wa Yanga wa hovyo kuna wengine kama sisi tuliozaliwa mjini tunajua nini maana uzalendo, kwa mwenye akili timamu katu hawezi kuishangilia timu ya nje ya Tanzania wakati unajua fika kuwa kufanya vizuri kwa club ya Tanzania ni manufaa kwa taifa lote, kuombeana mabaya tuombeane kwenye ligi yetu tu na sio kimataifa
ReplyDeletemimi naishi South Africa nilikua naangalia game la Simba na Chiefs baba mwenye nyumba wangu ni shabiki mkubwa wa Piretes yeye alikua anaiombea Chiefs ishinde na iliposhinda alinitania sana na kuniambia kuwa Tanzania hatujui mpira hatuna uwezo wa kuifunga timu yeyote ya South, ebwana sio siri iliniuma sana huyu jamaa ni mzalendo ila sisi hatuna uzalendo, NAITWA YUNUS AU BABA AZAD
ReplyDeleteTatizo Yanga wanachukulia utani wa jadi kama vita
ReplyDeletePenye ukweli tuseme tu ukweli sasa ikitokea hamjachukua FA mtasemaje maana VPL washachukia wenyenalo
Cha msingi mashabiki msiwe Kama nyie ndo wachezaji mnaongea Sana mpaka mnaharibu utaratibu Simba na yanga ni timu zetu zote penye kuzikosoa tukosoe tusitangulize ushabiki sana maaana lengo ni kuhakikisha Tanzania inasikika ulimwenguni kote. Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki Africa ameni
ReplyDeleteLa msingi nikuombeana wote nana yanga nawashangaa ikatokea hawajabeba ubingwa wowote watasema hawajabebwa alafu mbaya zaudi wajikute wako nafasi ya tatu waishukuru simba mana sisi simva makombe yote ya ndan tunayataka so wapamvane aidha waingiefainal tuwabutue waende au wamalize nafasi ya pili
ReplyDeleteKama ni kubebwa basi kamchukueni namungo hatutaki sisi. Anaenda mtu kulingana na nafasi aliyopo coz ingekuwa ni option musingemchukua yanga
DeleteSababu zimewekwa wazi kwamba kuweza kupata timu nne ni kwa sababu Simba imeweza kufika robo finally huyu kiongozi wa Yanga aache ujinga
ReplyDeleteNazani uzalendo ni tofauti Sana unapozifikiria Simba na yanga...mawazo ya wengi yameishia hapo..mbona Amna anateseka mtibwa au gwambina kwani sio timu zetu....ningefrai Sana atikee meekezaji aweke nguvu kwenye timu zingine tofauti na izi ambazo zimetujaa akilini.
ReplyDeleteSasa wewe unateseka nn na yanga .
ReplyDeleteSimba mwenyewe mpaka Sasa ivi bado haja qualify kucheza champion
ReplyDeleteSimamisha ligi alafu utajua kwamba amequalify au bado,inaonekana hujui lolote wewe mbumbumbu mzungu wa karata au garasa.
Delete