May 24, 2021


UONGOZI wa Yanga umewataja wachezaji wa Simba ambao wanastahili kucheza timu kubwa zaidi kutokana na uwezo ambao wameuonyesha katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hiyo ni kutokana na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kutinga hatua ya robo fainali na kutolewa na Kaizer Chiefs kwa jumla ya mabao 4-3.

Katika mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa FNB Soccer City Simba ilikubali kichapo cha mabao 4-0 na walikuja Uwanja wa Mkapa ngoma ilikuwa Simba 3-0 Kaizer Chiefs jambo ambalo limewafanya Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kimataifa kutolewa jumlajumla.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, (CEO), Senzo Mbatha ambaye kwa sasa yupo ndani ya Yanga akiwa ni mshauri kuelekea mabadiliko amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi kwa walichokifanya huku wakiwa wanastahili pia kucheza katika klabu kubwa zaidi.

 Wachezaji aliowataja ni pamoja na beki wa kati Serge Wawa, kipa namba moja Aishi Manula, kiungo Clatous Chama, beki Shomari Kapombe na Luis Miquissone ambaye naye pia ni kiungo kwa kueleza kuwa wanastahili kucheza klabu kubwa zaidi.

Senzo amesema:"Heshima zote kwa wachezaji niliofanya nao kazi, ukitazama walichokifanya kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Manula, Wawa,Luis, Kapombe na Chama wanastahili timu kubwa zaidi,". 

Naye Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz aliandika kwamba:"Kufuzu mchezo! Ila pongezi kwenu kwa kupambana kwa uwezo wenu wote ule ila nne zilikuwa nyingi," .


13 COMMENTS:

  1. Ukisikia ujinga ujinga ndio huo.Yeye Simba inamhusu nini?Atathimini timu yake hiyo mbovu.Timu imecheza mechi 4 zaidi ns bado imeshindwa kuongoza ligi.Haji Manara akiongea mnasema anaingilia huyu na Nugaz wanafanya nini???

    ReplyDelete
  2. sasa kwani kuna neno gani baya hapo mtani mpaka yanakutoka maneno kama hayo punguza jazba mtani wangu kwani si wamewasifu wachezaji wa timu yako alafu ukiangalia ni kweli wachezaji wa Simba wamecheza vizuri kweli mtani sisi ni watani na sio maadui am sorry if I offend u mtani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umenena vema

      Delete
    2. Mie namshangaa huyo mtani, mipovu yote ya nini? Michezo si uadui. Badilikaaaaa

      Delete
  3. Pelekeni unafiki huko.Utani kwenu umekwisha umebaki uadui na uhasama.Mafanikio ya timu mojawapo huko nyuma yalikuwa chachu ya timu nyingine kufanya vyema.Watu walikuwa wanataniana na kuzikana.Tokea waje wakuja kwenye uongozi wa Yanga na wapenzi wengi wasiojua utani mpira umekuwa uadui.Kabla ya ushamba wenu hakuna timu ilikuwa inapokelewa Airport.Ujinga huu mmeanza nyinyi halafu mnakuja ku comment kuhusu wachezaji wetu.Hiyo sio siri tuna wachezaji wazuri lakini kusema wanastahili kucheza timu kubw zaidi ni unafiki.Simba ni mojawapo ya timu kubwa sasa Afrika.Ushahidi ni imetoa wachezaji 5 kwenye timu ya wiki kwenye michuano ya CAF.Hakuba timu ya Tanzania inayo uwezo huo.Simba ni timu kubwa Afrika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. UNACHUKIA YANGA KUWASHANGILIA KAIZER NA UMESAHAU KUA SIMBA WALIINGIZA NUSU YA UWANJA WA MKAPA ILI WAMSHANGILIE AL AHLI DHIDI YA YANGA HADI WAMISRI WALISHANGAA !!!
      HUA HAMUWEKI KUMBUKUMBU AU ULIKUA HAUJAZALIWA !!

      Delete
  4. Wenyewe Yanga wana wachezaji wangapi wanaoweza kucheza nchi za nje? Senzo angeanza kutathimini hapo.

    ReplyDelete
  5. Labda nasema labda Mukoko Sasa hivi wanatafuta sababu ya kutocheza tarehe 3 Julai.Wapenzi wao wanasema wasipeleke timu wadai kanuni.Safari hii wakiingiza timu tunaficha funguo za basi.Hakuna kukimbia.

    ReplyDelete
  6. Kushangilia sio tija.Kwenda kuwapokea na viongozi wenu uchwara kuvaa jezi za timu za nje ni ulimbukeni.Niletee picha ya kiongozi wa Simba amevaa jezi ya Ahly ikicheza na Yanga siku hiyo nitajua tuna viongozi wazembe.
    Hakuna timu duniani isipokuwa hii yenu viongozi wanavaa jezi za timu zinazoshindana nazo.Nichukie ujinga.Nawaonea huruma hamjui mfanyalo.

    ReplyDelete
  7. huu mpira kaka hata huko kufanya kwako vizuri sio kama utafanya vizuri milele mtani kuna siku timu yako itakua sio nzuri na itakua nzuri timu nyingine kama unavyoona ulaya wako wapi Barcelona Liverpool na Fc Beyern Munchen mtani kuimba kupokezana waache hao washamba wasiojua maana ya Yanga na Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakupa kongole mtani. Hongera. Tunahitaji utani wenye mitazamo ya hivi. Safi Sana.

      Delete
  8. Shida Wapenzi humu wanamama hawana Baba yaani Baba hajafa ila Mama anamficha mtoto Baba kwa kuwa aliwapa wengi,nasema hv kwani mtu wa Yanga akisifia Simba inakukwaza Nini? Brother.

    ReplyDelete
  9. kwani hakuna watu waliozaliwa baba moja mama moja kisha mmoja anapenda Yanga na mwengine anapenda Simba watani zangu Simba tafadhalini musiwasikilize hao wanaochukulia Simba na Yanga kuwa maadui musishughlike nao' kumbuka hata gunia la viazi haviwezi kuwa viazi vyote vizima lazima utakuta vingine vimeoza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic