GEORGE Lwandamina, Kocha Mkuu wa Azam FC ana uhakika wa kuendelea kupata huduma za nyota wake wawili ambao wamehusika kwenye mabao 28 kwenye Ligi Kuu Bara baada ya mabosi hao kuwapiga pini nyota hao.
Juni Mosi, Prince Dube aliongeza dili la miaka miwili na atadumu mpaka 2024 yeye ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 14 na pasi tano za mabao.
Ayoub Lyanga,Juni 3 aliongeza kandarasi ya miaka miwli ambapo mkataba wake utameguka 2024. Nyota huyo kwenye ligi ametupia mabao 7 na pasi mbili za mabao.
Jumla nyota hao wamefunga mabao 21 na kutoa pasi 7 hivyo wamehusika katika jumla ya mabao 28 kati ya 44 ambayo yamefungwa na timu hiyo.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 30 na ina pointi 60 kinara ni Simba mwenye pointi 67 baada ya kucheza mechi 27.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC,Abdulkarim Amin amesema kuwa lengo la timu hiyo ni kuwa kwenye ushindani na kufanya vizuri katika mashindano ambayo watashiriki.
0 COMMENTS:
Post a Comment