June 2, 2021


IMEELEZWA kuwa mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewasili nchini Tanzania Jumanne, Juni Mosi, 2021 jioni baada ya kukaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa sasa.

 

Manji alikuwa akitajwa kuwa wakati wowote atarejea nchi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Taarifa zinaeleza kuwa alihojiwa kwa muda kadhaa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wake wa kuingia nchini.

 

Imeelezwa kuwa baada ya kutoa maelezo yake, aliachiwa baada ya maofisa hao kujiridhisha kuwa Manji ni Mtanzania na anayo haki na uhalali wa kuingia nchini Tanzania.

4 COMMENTS:

  1. Ina maana hao maafisa hawajui kuwa Manji ni myanzania? Je alikuwa diwani Mbagala kutokea taifa jingine? Ikiwa kilichoandikwa humu ni kweli basi tuna safari ndefu sana kwa aina hii ya watumishi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka labda nikueleweshe kidogo hapa, mimi nilishawahi kuwa Afisa Uhamiaji wa ngazi ya juu kabisa kabla sijabadili taaluma na kwenda kuwa mhadhiri. Sheria ya Uhamiaji ya Tanzania No. 7 ya mwaka 1995 hairuhusu mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili. Hivyo, naamini walitaka kujiridhisha sababu ya huyu mtanzania mwenzetu kusafiri na kukaa nje ya nchi miaka kadhaa- huenda alienda kwa matibabu, masomo, likizo, n.k. Hivyo, kuna haja ya kujirishisha kwamba yeye pamoja na familia yake sio raia wa nchi nyengine pia. Sababu nyengine ni za kiusalama wa nchi. Hii ikusaidie tu kutafakari zaidi.

      Delete
  2. Kwaiyo leo manji sio mtanzania kwaiyo niraia wawapi tuambieni bc mwenye ufahamu huo

    ReplyDelete
  3. sisi magumashi kila idara banaaa kkkkkkkkkkk Tanzania kwa magumashi nooma

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic