June 2, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao wawili wameondoka tayari katika kikosi hicho kwa ajili ya kujiunga na timu zao za taifa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa tayari wachezaji hao wameshakwenda nchini kwao huku wale ambao wameitwa timu ya taifa ya Tanzania, taifa Stars watakuwa kambini kwa muda mpaka muda wa kuripoti kambini utakapofika.

"Mukoko, (Tonombe) na Yacouba, (Songne) hawa tayari wamekwisha ondoka kwenye timu na kwenda kujiunga na timu zao za taifa.

"Wengine ambao wameitwa timu ya taifa hawa watakuwa kambini na wataondoka kuelekea kambini pale siku itakapowadia wakitokea kambini," amesema.


Wachezaji wa Yanga ambao wameitwa timu ya taifa ni pamoja na Metacha Mnata, Dickson Job, Lamine Moro na Feisal Salum.

Tonombe yeye ameitwa timu ya taifa ya Congo na Yacouba ameitwa timu ya taifa ya Burkina Faso.

  


6 COMMENTS:

  1. Lamine Moro ameitwa Taifa Stars?Kweli hawa makanjanja hawana aibu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaaa, hamna waandishi humu ni Utopolo mtupu

      Delete
  2. Keeli wachezaji Hao wanazo is a sifa za kuichezea timu ya taifa au kuwaridhisha tu wssisnze kufunguwa mashitaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic