WINGA wa klabu ya soka ya Inter
Milan na timu ya taifa ya Croatia, Ivan Perisic anatarajiwa kuukosa mchezo wa
hatua ya 16 bora dhidi ya Hispania utakaopigwa kesho, kufuatia kukutwa na
maambukizi ya virusi vya Corona.
Jana Jumamosi jioni Shirikisho la
soka la nchini Croatia (CFF), lilithibitisha taarifa za Perisic kukutwa na maambukizi
ya virusi vya Corona. Huku nyota wengine na wafanyakazi wa kikosi hicho wakipimwa
na kukutwa hawana maambukizi.
Nyota huyo Jumanne iliyopita alifunga
bao katika ushindi wa mabao 3-1, walioupata Croatia dhidi ya Scotland uliowapa tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro mwaka huu kutokea
kundi D.
Taarifa ya CFF ilieleza: “Shirikisho
la soka la Croatia Jumamosi jioni lilipokea majibu ya vipimo vya wachezaji wote
ambayo yalieleza kuwa mchezaji, Ivan Perisic amekutwa na maambukizi ya virusi
vya Corona.
“Perisic aliondolewa mara moja
kikosini na kutengwa na nyota wengine kwa ajili ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa,
na sasa atakuwa na siku 10 za kujitenga.”
0 COMMENTS:
Post a Comment