June 27, 2021

 


BAADA ya kikosi cha Simba jana Juni 26 kukamilisha mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC, leo Juni 27 kikosi kimerejea Dar.

Ubao wa Uwanja wa Majimaji ulisoma Azam FC 0-1 Simba na kuwafanya mabingwa hao watetezi kutinga hatua ya fainali.

Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi ambao walikuwa ni wakazi wa Songea pamoja na maeneo jirani ikiwa ni Mafinga, Iringa, Makambako na Njombe.

Alikuwa ni Luis Miquissone dk 89 aliyepachika bao la ushindi akitumia pasi ya Bernard Morrison kwa faulo ya harakaharaka iliyomshinda mlinda mlango namba moja Mathias Kigonya. 

Kwa sasa wachezaji wamepewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea kambini rasmi kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga, Julai 3, Uwanja wa Mkapa.

6 COMMENTS:

  1. Tuache ushabiki na roho mbaya Simba lazima wapewe heshima yao. Niliungalia mchezo wa fainali ya Azam cup kati ya simba na Azam. Wachambuzi wetu kazaa wamejaribu kuuelezea mchezo kadiri ya uwezo wao ila mchezo husika unajielezea wenyewe Kama ulibahatika kuangalia. Kwangu Mimi nimegundua mambo muhimu matatu.
    (1)Uwanja haukuwa rafiki kuwezesha kuonekana kwa mchezo uliokusudiwa kuchezwa na timu zote mbili ila umahiri,uwezo na umakini wa hali ya juu wa wachezaji wa Simba unakaa unajiuliza hiki kiwango Simba wamekifikia vipi Kama timu ya Tanzania? Kwangu Mimi mchezo ilikuwa wa upande mmoja mwanzo mwisho kwa maana yakwamba Azam walitumia muda mwingi kujilinda na labda waliegemea kwenye mikwajuu ya penalty zaidi kupata matokeo.
    (2)Azam wapo vizuri zaidi kuliko Yanga kitimu ila wanahitaji mechi nyingi za kimataifa kuwa Bora zaidi.
    Azam Wachezaji wao wengi wanakosa sharpness awareness ya mchezo na wasiuchukulie poa hata kidogo mchezo Kati yao na Simba Kuna mengi ya kujifunza Kama Wana nia ya kuja kufanya vizuri kimataifa.
    (3) Piga ua bila ya kusikiliza kelele za baadhi ya wadau wa soka kua Simba washambuliaji waliokuwa nao wanatosha, kwangu Mimi hapana Simba lazima wapige hatua nyengine kutafuta mshambuliaji wa viwango zaidi kuliko walikuwepo pale.Na mkubali zaidi Mugalu licha kuwa na baadhi ya mapungufu na Kama anguwepo Jana pangechimbika zaidi.
    Simba wamuongezee mkataba Morrison wasimchukulie poa hata kidogo ni kifaa kile kweli kweli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe hujaangalia mpira kama wachambuzi wengi walivyo, wawa aliruhusiwa apige mateke hadi ya kichwa kuwatoa azam mchezon lkn ktk wote hakuna aliyeliona hilo wazee wa miamala

      Delete
    2. aggrey morris ulimuons au ushabiki maandazi?

      Delete
  2. Hata like Goli haikuwa faulo Ni Kona yule left back alicheza Mpira,hayo ya ushauri nenda Wambie Kamati zao za Usajili.

    ReplyDelete
  3. Sema Refa alijitahidi kuweka vizaa Karibu na Goli la Azam akijua Kuna moja itatiki Mpira wa Karibu na Goli unaruhusu ianzishwe vile ,ikizingatiwa ule Mpira ilitakiwa uwe Kona
    .Baadae utasikia Kipyenga

    ReplyDelete
  4. Hizi mbeleko ziteketezwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic