SASA ni rasmi mchakato wa mabadiliko ndani ya Yanga utanedelea kama kawaida baada ya leo kupitishwa na wanachama.
Kupitia mkutano wa Wanachama ambao unafanyika leo Juni 27 Wanachama wa Yanga wamepitisha Mabadiliko ya Katiba yatakayowawezesha kufanya marekebisho ya Mfumo wa uendeshaji.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa hakuna Mwanachama aliyepiga kura ya hapana kupinga mabadiliko hayo, tasfiri yake ni kwamba mabadiliko hayo yamepitishwa kwa asilimia mia moja.
Mbali na hilo pia kuna wajumbe ambao wamependekezwa kuwa katika baraza la wadhamini.
Waliopendekezwa na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Yanga leo Juni 27, 2021 kuwa ndo baraza za jipya la wadhamini wa Klabu hiyo nipamoja na George Mkuchika, Geofrey Mwambe, Abbas Tarimba, Mama Fatma Karume na Mwigulu Nchemba
0 COMMENTS:
Post a Comment