TIMU ya taifa ya England imeinga hatua ya fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ya taifa ya Denmark kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali baada ya kuyeyusha miaka 55 bila kutinga katika hatua hiyo mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 1966.
Ni Mikkel Damsgaard alianza kuwatungua England dk 30 kwa pigo huru kwenye mashindano hayo lakini lilisawazishwa na Simon Kjaer ambaye alijifunga dk 39. Mpaka dk 90 za awali zinakamilika ubao ulikuwa unasoma 1-1 ilibidi England wasubiri mpaka dk ya 104 mbele ya mashabiki 60,000 nahodha Harry Kane alipachika bao la ushindi likiwa ni bao lake la 10 kwenye timu ya taifa.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Wembley ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo vijana wa Kocha Mkuu, Gareth Southagate ilibaki kidogo wafike hatua ya penalti kutokana na kufika katika dakika za nyongeza.
Sasa watakutana na Italia ambao walishinda kwa penalti 4-2 mbele ya Hispania baada ya kufungana bao 1-1. Mchezo huo wa fainali ambao utaamua nani atakuwa bingwa wa Euro 2020 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Wembeley, Jumapili.
0 COMMENTS:
Post a Comment