July 14, 2021

 


TANGU Jumapili iliyopita stori kubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa ile ambayo tunaifuatilia sisi wapenzi wa mchezo wa soka hapa nchini, ishu kubwa imekuwa ni suala la ujio wa basi jipya la klabu ya soka la Yanga.

Basi hilo tayari limewasili Tanzania na kuna uwezekano mkubwa kwa sasa likawa gereji kwa ajili ya kulifanyia maandalizi ya mwisho, ikiwemo kuliwekea stika za matangazo ya wadhamini wa klabu hiyo tayari kwa ajili ya kuanza kutumika na wachezaji wa klabu hiyo.

Basi hilo aina ya Scania Irizar limetolewa na mdhamini wa klabu hiyo mfanyabiashara, Ghalib Said Mohammed anayejulikana zaidi kwa ufupisho wa jina lake ambao ni GSM.

Ndinga hilo linatajwa kumgharimu bosi huyo kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 900 za kitanzania, huku hesabu yake mpaka itakapotoka gereji ikitajwa kufikia Shilingi Bilioni moja na ‘chenjichenji’.

Kwanza kabisa naupongeza uongozi wa Yanga pamoja na mdhamini wao GSM, kwa kuendelea kufanya mapinduzi mbalimbali ya kiudhamini wa klabu hiyo ambao unazidi kuongeza thamani ya kikosi hicho.

Huu ni mwendelezo wa mambo mengi mazuri na yenye manufaa makubwa kwa soka la Tanzania, yanayoendelea kufanywa na Yanga chini ya udhamini wa GSM. Chini ya mfanyabiashara huyo tumeishuhudia Yanga ikifanya maboresho makubwa ya kikosi chao kwa usajili wa wachezaji wengi bora mwanzoni mwa msimu uliopita.

Lakini GSM pia ndiyo ambao wamejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa mabadiliko ya kiundeshaji wa klabu hiyo kwa kutoa fungu la fedha za kuwezesha mchakato huo, kuanzia hatua za awali mpaka ulipokamilika, na kupitishwa kwenye mkutano mkuu wa Wanachama wa Yanga uliofanyika Juni 27 mwaka huu.

Lakini pia ni chini ya uongozi huo tumeona Yanga ikifanikiwa kusaini makubaliano ya kimkataba wa haki za matangazo ya Televisheni na kampuni ya Azam Media, wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.8 za Kitanzania.

Kwa watoto wa mtaani hii tunaiita gari limewaka, bila shaka kuna mengi yanatarajiwa zaidi, kwa ajili ya furaha ya mashabiki wa klabu hiyo kongwe ambao kwa sasa hawashikiki kwa ‘kujimwambafai’ huku mitaani.

Mashabiki wa Yanga kwa sasa wanaonekana kuzidiwa na furaha ya vifurushi vya zawadi za furaha wanavyopokea, walianza na ushindi dhidi ya Mtani wao Simba, wakapata mabilioni ya Azam, na sasa basi jipya.

Kutokana na kelele za Yanga na basi lao jipya, mashabiki wa Simba nao wamekuwa wakiwajibu kiutani Yanga kuwa, wasijisahaulishe na basi jipya wakati Injinia aliwaahidi ubingwa.

Kwangu nadhani kuna pointi kubwa ambayo inatoka kwenye utani huu, kwani mwanzoni mwa msimu huu kulikuwa na kauli mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Yanga kuhusiana na malengo yao ya kushinda kombe la Ligi Kuu Bara.

Mfano ni pale Ofisa mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz aliyeahidi Yanga wangetwaa ubingwa kabla ya michezo yao 10 ya mwisho.

Labda zilikuwa tambo tu, lakini tukirejea kwenye uhalisia ni wazi ubingwa wa Ligi Kuu ni miongoni mwa mahitaji makubwa ya Yanga kwa misimu minne mfululizo sasa.

Jambo la kujiuliza zaidi kao ni kwamba, katika kipindi chote hiko ni Mtani wao Simba ndiye amekuwa mtawala wa kombe hilo.

Heshima ya klabu yoyote duniani, ni ubora walionao katika kutawala soka la nchi ambayo klabu hiyo inatoka (kwa kutwaa makombe), na tunaona hili kwa klabu kama Bayern Munich ya Ujerumani, Al Ahly ya Misri na nyinginezo.

Hii pia hutoa faida ya bingwa kuwa mwakilishi wa nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, hivyo ishi ya Simba kutangaza ubingwa kwa misimu minne mfululizo si jambo la kuchukuliwa poa kabisa na wadau wa Yanga.

Kuna msemo usemao ‘acha mvua inyeshe tuone panapovuja’, hii ina maana kwamba hii mvua ya utawala wa makombe ya Ligi Kuu huko Simba, inadhihirisha kuna mahali pale Yanga kunavuja.

Katika hili uongozi wa kikosi cha Yanga unapaswa kukaa chini na kuangalia ni wapi wanakosea hatua, kiasi cha Mtani wao kujimilikisha makombe kila kukicha.

Ifike wakati waambizane ukweli na kuacha kufichana, ni kweli basi jipya ni muhimu sana Yanga, lakini lisitumike kuwasahaulisha mashabiki wa Yanga juu ya ahadi ya ubingwa mliowapatia.

Injinia Hersi, naomba unisaidie kumwambia bosi Ghalib Yanga wanahitaji ubingwa kuliko wanavyolihitaji basi jipya.


Uchambuzi wa Vuvuzela unaopatikana kwenye gazeti la michezo la Championi kila Jumatano

13 COMMENTS:

  1. Unaweza ukapata ubingwa bila kuwa na resources za kutafuta ubingwa? Au umeandika baada ya kushiba wali maharage,,unadhani yanga inaviongozi vilaza kama wewe,,,,usiandike kitu kwa mihemuko na ujinga wa kiwango cha juu namna hii.

    ReplyDelete
  2. Haukukosea kabisa kujiita VUVUZELA;nina wasiwasi unawaza kwa kutumia misuli ya makalioni na sio kwa kutumia misuli ya akili.Unadhani bila ya kuwa na miundombinu wezeshi huo ubingwa utapatikana vipi,inawezekana kabisa siku nyingine utakuja na maoni ya kuwataka Yanga wasiwasajili wachezaji wote walionao kisa tu uongozi uliahidi ubingwa lakini hawakufanikiwa kuuchukua hivyo wasiwasajili.Kutokamilika kwa malengo fulani hakuzuii kukamilisha malengo mengine vinginevyo ukiendekeza hiyo imani uliyonayo utajikuta unabaki hapo hapo na kuanza kuwatafuta watu uchawi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Halafu ubingwa wa simba haupati uwanjani anaupata nje ya uwanja kama yuko vizuri mbona yanga haifungi ubingwa wa miundo mbinu

      Delete
    2. Kwahiyo sisi tuishie kumfunga Simba wakati yeye anachukua ubingwa?

      Delete
    3. Kwa hiyo na Yanga wameamua kuiga kwa kuutafuta ubingwa nje ya uwanja, yaani barabarani yanakopita mabasi?

      Delete
  3. Utopolo endeleeni na ujinga huo huo mpaka mtakapo amka mkute Simba yuko mbali sana... Kama hakuna resource walioahidi ubingwa walikuwa wanadanganya au? Kama Simba inashinda kwa miundo mbinu basi Utopolo inajua zaidi miundombinu kuliko Simba ndo maana wakaifunga, Kama ni hivyo mmekosaje ubingwa? ...... Utopolo, Utopolo, Utopolo mnajichelewesha wenyewe

    ReplyDelete
  4. Waandishi wa bongo hata hawajui kwann wanaandika, wasipokua na resources za kutosha watachukuaje ubingwa au ndio ukanjanja wenyewe, hata hao Global publisher wasipokua na vitendea kazi watafikiaje malengo?
    You have to write common sense, rather than Nonsense

    ReplyDelete
  5. Mimi ni shabiki wa Simba lakini habari hii mbona haileti maana. Kila jambo linapangiwa utaratibu na bajeti yake. Unahitaji gari (bus) zuri la kusafiria wachezaji lakini pia unahitaji maandalizi mazuri ya timu kuweza kushinda. Yote hayo yanaganyika na timu zote hususan Yanga, Azam na Simba. Sasa tatizo lako mwandishi ni nini? Hivi wewe unajua sana vipaumbele vya Yanga kuliko GSM? Sio sahihi kuingilia mipango ya klabu kiasi hicho. Tuwape heshima wanaojitoa kufanya jambo zuri kwa klabu zetu na si kubeza jitihada zao.

    ReplyDelete
  6. Mwandishi bila kupepesa macho hapa umepuyanga. Usafiri ni kiwejeshi mhimu katika mikakati ya kuwa bingwa. Chukulia mfano unahitaji kwenda kucheza Dodoma na una usafiri mbovu umechelewa kufika na hivyo wachezaji wanatumia muda mrefu njiani wanafika dodoma kwa kuchelewa wanashindwa kufanya kuendelea na program ya mazoezi waliyojipangia kwa uchovu...wanaingia uwanjani kichwa kichwa halafu wanapoteza mchezo alama zinakosekana, huo ubingwa wataupataje? Iliwahi kutokea basi la Yanga kuharibika njiani mengi yalisemwa na waandishi kama wewe mkiuliza inakuwaje Yanga Wana gari bovu? Leo gari limepatikana mnalalamika, tuwaeleweje? Hivi elimu zenu haziwafundishi ku-think critically?" Yaani hapa umejionesha jinsi ulivyo mweupe kichwani katika kupanga mipango ya mafanikio. Kwa ufupi kwenye mafanikio hakuna short-cut rahisi kama unavyolazimisha. Idiot!

    ReplyDelete
  7. mnamshambulia mwandishi sana mnasahau kuwa jamaa hajajibu ameukosaje ubingwa alioahidi!
    alisema yanga ikikosa ubingwa niulize mimi (GSM )
    sasa mnataka asiulize wakati jamaa alisema aulizwe?

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWANI SIMBA WALIMUULIZA NANI WALIPOKOSA UBINGWA TANGU MWAKA 2013 HADI 2017 ?

      Delete
  8. Nadhani timu iliyoichukua ubingwa mara nyingi zaidi Tanzania inajulikana!!! Suala la msingi ni umeufanyia nn ubingwa uliochukua nadhani klabu zetu zinahitaji maboresho makubwa ya miundombinu kuliko ubingwa wa ligi kuu na hapa muandishi ilitakiwa uitaje azam sio yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic