July 14, 2021


 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa kijana wake Bukayo Saka atakuwa imara na kurejea kwenye ubora wake kwa kuwa amepokea upendo na sapoti kutoka katika ulimwengu wa mpira sio kutoka ndani ya Arsenal pekee bali ulimwengu mzima.



Kocha huyo wa Arsenal amesema kuwa alipata muda wa kuongea na mchezaji huyo raia wa England ambaye alikumbwa na suala la ubaguzi wa rangi baada ya timu yake ya taifa ya England kupoteza katika mchezo wa fainali ya Euro 2020.



Mbali na Saka mwenye miaka 19, Arteta alipata muda wa kuzungumza na washkji zake wengine ambao ni Marcus Rashford na Jadon Sancho ambao wote walikosa penalti Uwanja wa Wembley Jumapili jambo lililofanya washambuliwe katika mitandao ya kijamii kwa kuwa walifanya timu yao ikose ubingwa wa Euro .

Suala hilo la ubaguzi wa rangi limepokewa katika hali ya kipekee ambapo chama cha soka cha England kiliweka wazi kwamba kitafuatilia suala hilo huku Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate,  Waziri Mkuu, Boris Johnson wamekuwa mstari wa mbele kupinga suala hilo.


"Nilipata muda wa kuongea na Saka nilimwambia kwamba anaweza kuwa imara. Kwa kile ambacho alipewa afanye kwake kilikuwa kikubwa hivyo ninamwamini na ninajua kwamba atarudi kwenye ubora," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic