July 14, 2021


 INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga, beki Shabani Djuma ameweka wazi kuwa atapambana kuona timu hiyo inasepa na taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Raia huyo wa Congo ambaye ni mali ya Yanga akiwa amekamilisha dili la usajili wake kwa kandarasi ya miaka miwili anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho hivi karibuni.

Anaibuka ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi akitokea AS Vita ambapo huko alikuwa ni moja kati ya manahodha wa timu hiyo.

"Kila kitu kuhusu Yanga kwa sasa ninakifuatilia na nafahamu kuwa imepita muda mrefu bila Yanga kutwaa ubingwa wa ligi ambao umekuwa ukienda Simba.

"Nitahakikisha kwamba napambana na kushirikiana na wenzangu katika kuona kwamba tunaweza kutwaa ubingwa wa ligi na ninajua kwamba haitakuwa kazi nyepesi," amesema.

Simba imetwaa ubingwa mara nne mfululizo ambapo msimu huu imetwaa taji hilo ikiwa na mechi mbili mkononi na inatarajiwa kukabidhiwa kombe hilo Julai 18, Uwanja wa Mkapa.

Siku hiyo Simba itacheza na Namungo FC ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.

3 COMMENTS:

  1. Tatizo la watu wansosajiliwa yanga au uongozi wa yanga ni lilelie, makelele mengi kabla hata ya kuingia uwanjani. Hiyu nae kaanza. Kila siku jembe jembe, kpleo, koleo, shoka shoka ili mradi hadi inachosha. Wewe njoo uonekane kazi yako uwanjani.

    ReplyDelete
  2. Kwani himjui wewe Nani aonekane kwa Nani Malaria mkubwa

    ReplyDelete
  3. Jembe limevunjika mpini.... Labda mapinduzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic