RASMI mabosi wa Yanga wamekamilisha dili lao la kumsainisha nyota wa AS Vita, Djuma Shaban kwa kandarasi ya miaka miwili.
Hivi karibuni Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga alikwea pipa kuelekea DR Congo ambapo ilielezwa kuwa alimalizana na baadhi ya nyota ikiwa ni pamoja na Djuma.
Picha ambazo zimesambaa leo katika mitandao ya kijamii zimemuonyesha beki huyo akimwaga wino na moja akiwa na Injinia.
Kuhusu usajili wa msimu huu Injinia aliweka wazi kwamba watafanya usajili mzuri ambao utakuwa ni wa kisasa kabisa.
Taarifa zimeeleza kuwa nyota huyo atajiunga na Yanga msimu ujao wa 2021/22 atatambulishwa rasmi siku ya Wananchi.
Kumbe ilikuwa bado
ReplyDeleteKila kitu ni mchakato sio kama kwenda kukata tiketi ya mwendo kasi kisha unasubiri basi lije.
DeleteMtaMshia michakato kila mwaka wenzenu Wana wanatimiza malengo ya kubeba vikombe
DeleteKama alivyoletwa Chikwendeee
ReplyDeleteAu fiston, sarpong yikpe, na wengine waliovunja mikataba
DeleteHahah
ReplyDeleteHv Jana Chikwende hakuingia kabisa
ReplyDeleteAnasubiri kunyanyua makwapa Mara 2
DeleteHivohivo tu
ReplyDeleteSimba wajinga sana walianza oooh atuwezi kumchukua djuma now wamebadilika kuona kwanza yanga sio wamaneno kama yule msemaji wao sasa nyie jisahau mkazani kila mwaka nguvu ya wachezaji ni ile ile wanapugua kasi na wenzenu tunafanya usajili wa vijana, siku zote usijisifie huna mbio msifie na anayekukimbiza
ReplyDeleteSamahan wewe n wa kike au wa kiume?
DeleteNapata raha sana yanga 👋
ReplyDeleteMtuboreshee tu kikosi hatutaki maneno mengi.
ReplyDelete