July 13, 2021


 KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imetwaa mara ya nne taji la Ligi Kuu Bara na msimu huu wa 2020/21 imefanya hivyo ikiwa na mechi mbili mkononi.

2017/18 Simba ilitwaa ubingwa uliokuwa mikononi mwa watani wao Yanga waliotwaa taji hilo msimu wa 2016/17 baada ya kufikisha jumla ya pointi 68 na tuzo ya ufungaji bora ilikwenda kwa Simon Msuva aliyekuwa akikipiga Yanga pamoja na Abdulhaman Mussa ambaye yupo zake Ruvu Shooting baada ya kutupia wote mabao 14.

Msimu wake wa 2017/18 Simba ilitwaa ubingwa ikiwa na pointi 69 safu yake ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 62 huku ile ya ulinzi ikiokota kimiani mabao 15. Tuzo ya mfungaji bora ilikuwa mikononi mwa  Emmanuel Okwi alitupia mabao 20 alikuwa mali ya Simba.

2018/19 Simba ilitwaa ubingwa na pointi zake ilikuwa ni 93 safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 77 ile ya ulinzi ilifungwa mabao 15 na tuzo  ya mfungaji bora ilikuwa miguuni mwa Meddie Kagere aliyetupia  mabao 23 ni mali ya Simba.


2019/20 Simba ilitwaa ubingwa wake wa tatu ilikusanya jumla ya pointi 88 safu ya ushambuliaji ilitupia mabao 78 na ukuta wao uliruhusu mabao ya kufungwa 21 tuzo ya mfungaji bora ilikuwa ni kwa Kagere tena alitupia mabao 22 ni mali ya Simba.

Msimu wa 2020/21 ni Simba wamesepa na taji hilo wakiwa na pointi 79, safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 73 ule ukuta wao uliokota mabao 13 na mfungaji namba moja ni John Bocco mwenye mabao 15 mali ya Simba.

Mechi zake mbili ambazo wamebakiwa nazo ni dhidi ya Azam FC inayotarajiwa kuchezwa Julai 15 pamoja na mchezo dhidi ya Namungo FC ambao unatarajiwa kuchezwa Julai 18.

1 COMMENTS:

  1. Hii ndo Lunyasi hailazimishi furaha ohh mara tumenunua basi ohh mara Niyonzima day ni vitendo zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic