July 12, 2021


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa msimu huu watani zao wa jadi, (Simba) utakuwa ni wa mwisho kwao kuchukua ubingwa huku akifichua kwamba waliweza kuwafunga kutokana na mipango ya ndani na nje ya uwanja.

Ikumbukwe kwamba licha ya Simba kutangazwa kuwa mabingwa baada ya kucheza jumla ya mechi 32 walipoteza mechi tatu ambapo katika hizo moja walifungwa na Yanga.

Ilikuwa ni Julai 3 Uwanja wa Mkapa ambapo ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Zawad Mauya langoni alikaa Farouk Shikalo ambaye aliweza kuzuia michomo ya nahodha wa Simba, John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu.



Bumbuli amesema: "Unajua wenzetu kwa sasa hivi wanatabia ya kuwa na confindence, (kujiamini) kutokana na majina ya wachezaji walio nao lakini mpira hauchezwi kwa maneno ni dk 90.

"Sisi Yanga, kamati ya utendaji ilikaa na katika kipindi ambacho kamati ya Yanga ilikutana mara nyingi ni wakati huu mpaka nikauliza je hamvunji katiba? Wakaniambia kwamba hivi ni vikao vya utendaji.

"Kwa hiyo tulikaa tukajipanga, tukawaacha wao waendelee kuongea, waendelee kuota ubingwa, waendelee kuomba kuletewa kombe uwanjani. Kuhusu ubingwa wakibahatisha safari hii wakachukua hapa utakuwa wa mwisho," amesema.

Tayari Bodi ya Ligi Tanzania imewatangaza Simba kuwa mabingwa kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa pointi ambazo wanazo hazitafikiwa na timu yoyote. Unakuwa ni ubingwa wao wa mara ya nne mfululizo.

Bado wana mechi mbili mkononi ambazo ni dhidi ya Azam FC Julai 15 pamoja na ile dhidi ya Namungo FC, Julai 18.


Baada ya kumaliza mechi za kufunga msimu wa 2020/21 watakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni fainali itapigwa mwisho wa reli Kigoma, Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika.


8 COMMENTS:

  1. Masikini wanaropokwa bila ya kuweka akiba. Hao watafunga midomo hapo 25. Kwani fanikio gani la uhakika walilolipata hata wakajiamini? Wao akili zao wanahisi hizo kejeli zao zitakuwa na athari ya saikolojiya kwa Mnyama, watavunjika moyo na kushindwa. Yabwege

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa Maamuzi Yale ya refaree kwenye mechi ya Yanga na Simba na nyie waandishi hata aibu hamna kuupamba ushindi wa Yanga zidi ya Simba?Kwangu Mimi Maamuzi ya mechi ya mechi ya Simba na Yanga ni jitihada za makusudi za kuutukana mchezo wa mpira nchini na kuinajisi taaluma ya urefaree.

      Delete
  2. Si tuliambiwa yar 22 CAS itsipoka simba ubingwa, kulikoni tena wamenyoosha mikono? Au kwa vile tayari wamefanikiwa kuwazuga wapenzi wao kuhusu kukosa ubingwa? Haiwezekani, mwanzo wa musimu GSM alisemaje?

    ReplyDelete
  3. Mwakani tena tutaambiwa hivi hivi

    ReplyDelete
  4. Hawa akili zao zipo mfukoni, mdhamini wao asharopoka wasipochukua ubingwa msimu huu wamuulize na ubingwa wamekosa,
    Wanazidi kudanganywa na kujidanganya wanaume tuendelee kukusanya vikombe vyetu

    ReplyDelete
  5. je hakumbuki na mwaka jana Yanga walisema hivyo?eti watachukua makombe yote. na walianza na la mapinduzi.ni nini kimetokea..
    sababu za kikosi ni kipya hazina mshiko...mkisajili wa milioni 500 jua Simba naye anasajili wa mil 800.kila la heri

    ReplyDelete
  6. Jamaa hata hafikirii anachoongea, Yani mtu kachukua ubingwa halafu unasema anacheza mpira mdomoni... Kweli Utopolo ni Utopolo tu yaani tusiwalaumu

    ReplyDelete
  7. Utopolo hub ndo ubora wao hahahaha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic