July 14, 2021

 


UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Yanga umetamba kuendeleza moto wa ushindi katika michezo yao yote miwili iliyosalia ya Ligi Kuu Bara, dhidi ya klabu za Ihefu na Dodoma Jiji ili kuzidi kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.

Yanga inahitaji angalau pointi moja katika michezo hiyo miwili iliyosalia, ili kujihakikishia nafasi ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, ambapo watakuwa wanafikisha pointi 71, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote iliyo chini yao.

Yanga inatarajiwa kucheza na Ihefu kesho Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni. huku wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Desemba 23, mwaka jana.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Maandalizi yetu hayalengi timu moja pekee, bali tunajua ratiba yetu ina michezo miwili iliyosalia kwenye Ligi Kuu Bara, ambayo ni dhidi ya Ihefu, na Dodoma Jiji. Malengo yetu ni kushinda michezo hiyo ili kumaliza katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo.”

 

4 COMMENTS:

  1. Mkishinda moja tu ubingwa mnachukua tar 23

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Kama Mambo ya yanga yana kukera siunyamaze,sio laazima utolee maon

      Delete
  2. Kuna watu wakiona neno Yanga Fc wanateseka sana, tatizo la kuishi kwa kukaririshwa ubaya, wamebaki na chuki mpaka zinawadhuru

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mashabiki wengi wa Simba hawajui siasa za mpira aidha ni ushamba wa ushabiki au Haji Manara amewashikia akili zao.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic