August 23, 2021

 MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa walistahili ushindi katika mchezo wa jana ila walishindwa kutumia vema nafasi ambazo walizipata.



Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates ilikubali kunyooshwa kwa mabao 2-0 jambo lililowafanya wayeyushe mazima pointi tatu. 


Unakuwa no mchezo wa pili kwa Arsenal kupoteza kwa kuwa ule wa ufunguzi walipoteza mbele ya Brentford wakiwa ugenini.


Arteta amesema:"Ilikuwa ni lazima tushinde ila namna hali ilivyokuwa mambo yalibadilika. Kipindi cha kwanza tulikuwa na nafasi ya kushinda ila haikuwa hivyo.


"Walipopata bao wapinzani wetu walizidi kulazimisha kupata ushindi na waliweza kufanya kwa nguvu dakika zote 90 hivyo hamna namna ni mbaya kwetu na ukikumbuka kwamba tuliwakosa wachezaji wetu 8 ama 9 hivi,".

5 COMMENTS:

  1. Maneno ya kipuuzi. Wenzako wana possession ya 65 wewe 35 unastahili vipi kushinda? Kocha mwenye werevu hawezi kukitetea hivi. Wachezaji 8 uliokosa ni akina nani, sema huna timu imara. Kulazimisha kwa nguvu nini maana yake, walitumia vurugu? Ovyo kabisa.

    ReplyDelete
  2. Hawa ni kama Utopolo tu sema wao hawailalamiki TFF yao yaani FA ya England kwa kufungwa.

    ReplyDelete
  3. Mie naona kocha ameshindwa maana so kwa matokeo haya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic