August 5, 2021


 VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo kwenye Kombe la Kagame utakaocezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kikosi cha Azam FC kitashuka uwanjani kuivaa Messager Ngozi ya Burundi, katika mchezo wake wa pili wa Kundi B la michuano ya Kombe la Kagame, saa 10:00 jioni.


Viingilio vya mchezo huo ni Sh. 2,000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 5,000 kwa V.I.P. Katika kundi hilo Azam FC inaongoza ikiwa na pointi tatu baada ya kushinda mchezo wa kwanza mbele ya KCCA kwa mabao 2-0, Uwanja wa Azam Complex na yote yalifungwa na Peter.

Bahati amesema:"Tumejiandaa kufanya vizuri na tunajua kwamba utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa. Kikubwa ni mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," .

Mabingwa watetezi wa taji hilo la Kagame ni KCCA kutoka Ugnada na Azam FC imeweka wazi kwamba inahitaji kulitwaa taji hilo.

2 COMMENTS:

  1. Lakini matopolo wanaendelea kuhakikisha kuwa kombe ni lao

    ReplyDelete
  2. Nyie pambaneni na mechi ya Manara vs mudi na ubavu wake barabara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic