August 26, 2021

 


BREAKING:Rasmi Klabu ya Al Ahly leo Agosti 26 imemtambulisha Luis Miquissone kiungo mshambuliaji kuwa mali yao kuanzia msimu wa 2021/22.

Nyota huyo aliyekuwa anakipiga ndani ya Simba sasa ni rasmi atakuwa mali ya Waarabu hao wa Misri baada ya kukamilisha utaratibu mzima wa kupata saini yake.

Inaelezwa kuwa ni dili la miaka minne ambalo amesaini nyota huyo aliyekuwa akisumbua katika ardhi ya Tanzania huku guu ambalo akilipenda kutumia kuwa ni lile la kushoto.

Kwa msimu uliopita wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara alihusika katika mabao 19 kati ya 78 ndani ya Simba. Alifunga 9 na kutoa jumla ya paso 10.

Pia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,  Uwanja wa Mkapa aliwatungua Al Ahly bonge moja ya bao akiwa nje ya 18 kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama ambaye naye amesaini dili la miaka mitatu RS Berkane ya Morocco. Unajua

10 COMMENTS:

  1. Sijui ni kwa nini ukiwa shabiki wa utopolo ni rahisi kuchotwa akili. Haya nendeni siku ya wananchi mkatambulishwe hiyo Luis

    ReplyDelete
    Replies
    1. Injinia kasema hakuna linaloshindikana huenda akaja yanga kwa mkopo

      Delete
  2. Nani akukopeshe mchezaji wa gharama kiasi kile?

    ReplyDelete
  3. Hakuna mtu muongo kama Engineer kawa kamata utopolo balaa

    ReplyDelete
  4. Niliona ni jambo geni na la ajabu Luis alienunuliwa kwa mabilioni halafu Wamisri wamtoe kwa mkopo jambo haliingii akilini hata kidogo

    ReplyDelete
  5. Iv hapa wanaband fc wanajivunia nn mpaka watuambie kua cku ya wananch wanamtambulisha luis? kaz wanayo

    ReplyDelete
  6. Utopolo wanaendelea kuda ganywa na kwasababu ya ukapuku wanaendelea muwakubali wadhamini wao.
    Ukapuku mpya jamani unaendeshwa Kama Kali bovu nawe unasema ndiyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic