August 8, 2021



 

 RASMI hesabu za kumsajili kipa namba moja wa timu ya taifa ya Mali zimekamilika na atakuwa na timu hiyo msimu wa 2021/22.

Nyota huyo kutoka Mali, anaitwa Diarra Djigui ana umri wa miaka 26, na ni nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanaocheza kwenye ardhi ya nyumbani (CHAN) 2020.


Sababu kubwa ya Yanga kumpa dili kipa huyo ni kuwa chaguo namba moja la kocha wa Yanga, Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye amekuwa akitafuta kipa anayemtaka.


Kwa sasa Yanga ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi kwa kuwa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika pia wanahitaji taji la ligi.


Usajili wa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Mali unatoa nafasi kwa Faroukh Shikalo kuchimba mazima Yanga.

Nyota huyo amepewa dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

8 COMMENTS:

  1. Huyo atatakiwa kuichezea timu yake ya taifa wakati yanga inamuhitaji kugombea ubingwa wa Afrika

    ReplyDelete
  2. Kongole mtani umelamba dume na hapana shaka hakutakua na visingizio endapo utaukosa ubingwa msimu wa 2021/2022

    ReplyDelete
  3. Hamna kitu hapo hata shikalo ni kipa wa timu ya Taifa ya kenya.kipa hawi kipa mpaka aje kuthibitisha ubora wake.

    ReplyDelete
  4. Hata Metacha Mnata yupo juu zàidi ya huyo kipa

    ReplyDelete
  5. Yeye anachezeaga timu taifa tu hana klabu duu wandishi wakibongo noma

    ReplyDelete
  6. Aje bongo,, ht akiwa mzuri vp km beki mbovu ataokota mara nyng tu mipira wavuni

    ReplyDelete
  7. Bravo, ni kipa mzuri sana. Waache mikia wabaki na kiroba chao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic