STAA wa Simba, Clatous Chama, Agosti 6, 2021 ameonja joto la jiwe baada ya kuchenjiwa kibao na muwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kisa Haji Manara.
Chama akiwa Live Insta kwenye mkutano wake na mashabiki ambao Mo alikuwemo, aliulizwa swali kuhusu kuondoka kwa Haji Manara ndani ya Klabu ya Simba, kwenye kujibu Chama alimsifia Haji kitendo ambacho kilionekana kumchefua sana Mo.
Mo alimuuliza Chama “Haji ndiye aliyekulipia ada ya uhamisho?” Chama akiwa anamjibu Mo, alijibu kwa kuomba msamaha kama amemkwaza, Mo akamuuliza tena Nani aliyekulipia Ada….Haji? baadaye Chama alipotaka kujibu Mo akamwambia anatoka kwenye mkutano huo.
Ndani ya ligi nyota huyo amehusika kwenye mabao 23 akifunga mabao 8 na kutoa pasi 15 za mabao kati ya mabao 78.
Kwa sasa inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za Kaizer Chiefs pamoja na timu ya kutoka Morocco inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ya FAR Rabat.









Binadamu siku zote hatuwezi kuwa na mitizamo sawa haya yanayoendelea ni utoto na ufinyu wa fikira. Hakuna mkosaji katika uso wa dunia asiye na Mazurisambamba na mabaya yake hivyo sioni sababu ya mazuri yake kutosifiwa ama kutambuliwa
ReplyDelete!!!!
Auzwe mapema tu ni mchezaji mzuri ila amejiingiza kwenye siasa ambazo zinaweza kumvuruga uwanjani.Chama pengine hana kosa lakini alipaswa kufahamu au kufahamishwa yaliyotokea Kati ya Manara na bosi wake. Lakini hii pia inaonesha jinsi gani Manara alivyoamua kuvunja uhusiano wake na Mo na simba kwa ujumla kwa njia ya Uadui,hakika haikupaswa kuwa hivyo.
ReplyDeleteNa hakika kabisa bila ya Mo Manara na Chama wasingejuana,Mungu mkubwa.
Matatizo ya Haji Manara na MO au na Barbara sio matatizo ya Manara na Chama au na mchezaji mwingine yeyote ndani ya Simba.
ReplyDeleteImenikumbusha kauli ya rais wa kwanza wa Zambia marehemu Keneth Kaunda na kurudiwa na Nelson Mandela kwa Marekani na washirika wake walipowaambia sio lazima maadui wa Marekani wawe pia ni maadui zao na hivyo hivyo sio lazima marafiki wa Zambia wawe ni marafiki wa Marekani,Zambia itamheshimu yeyote anayewahehimu Wazambia na Waafrika kwa ujumla hata kama atakuwa ni fisi ili mradi anaheshimu hadhi na utu wao.
Mo asilazimishe kuwashikia wengine akili kisa tu yeye ndo anaetoa hela,thamani ya utu wa mtu haipimwi kwa fedha,awaache wengine wao na uhuru wa kujiamulia marafiki
Kwa wafuatiliaji wa mpira wa Bongo ,bora Chama aondoke upesi maana bench linamuita kuanzia next season sababu kagombana na mlipaji mkuu.Kwa wanaofatilia mpira ataanza kuwekwa bench halafu tutaanza washabiki kudanganywa kwamba kiwango chake kimeshuka na kwa kutumia waandishi vilaza tutaamini.Inabidi Wana Simba tumuombe sana Allah msimu ujao,maana Haji Manara ametumiwa na Utopolo kutuvuruga Wana Simba ili tuyumbe ili team ifanye vibaya.Lakini Mtego huu ambao Manara ameutumia utamfyatukia mwenyewe, maana alishagundulika siku nyingi.
ReplyDeleteChama jiangalie ndugu yangu fuata kazi iliyokuleta msimbazi usifuatilie mambo yasiyokuhusu
ReplyDeleteManara ni chui alijivisha ngozi ya kondoo. Hafai maana ni yanga alotopea. Ndio maana GSM wamekuwa wakifanikiwa kuihujumu simba kupitia manara. Tena manara huwa halipwi kitu na GSM. ni kutimiza wajibu wake kwa yanga. Na ndio maana wapenzi wa yanga baafa kuona pandikizi lao limengolewa simba wamechanganyikiwa. Manara muogopeni kuliko corona
ReplyDeleteAkili ya kupewa changanya na yako kwani yanga aliposhinda dhidi ya simba,simba haijachukua ubingwa??? Au mechi za yanga kushindwa kufanya vizur kwa mechi kadhaa dhidi y timu zingine nje ya simba ilo lilisababishwa na haji kwamba hakuwahujumu ...fikra finyu za kushikwa akili ndo hixo zinafanya kurithi uadui hata kama hakuna umuhimu wa kufanya ivo..watu ni pumbavu sana huumu...
DeleteMuda utaongea
ReplyDeletehaji kagombana na kiongozi wake kwa siri.kisha kiongozi kwa kujua halikubaliki,anapost voice note.hapo ndio haji anaposema wamenidhulumu sio pesa,bali nia ovu ya babra,halafu chama kaulizwa swali.ktk hadhara,kajibu kwa maoni yake.usiwaseme watu kwa mabaya.ukiniambia kutoa hisia zake ambazo ameshawahi kuzionyesha wakati akipokea tuzo siku zilizopita.ukiiangalia kimaskini,huyu anatupa mkate hiyo ndio ipo kichwani,akija bill gate hapo kati huyo moo tunamkimbiza.hivyo hatuangalii haki,hisia,maoni ya wengine.ndio maana tupo hapa,kwanza kwenye sheria zetu kukaa kimya ni kukubali makosa na kusema uongo pia ni makosa.
ReplyDelete