August 13, 2021


 CLATOUS Chama kiungo namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho anatajwa kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco kwa dili la miaka mitatu.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge ambaye alikuwa anafundisha AS Vita anatambua vema uwezo wa Chama kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 nyota huyo alitengeneza jumla ya pasi 15 na alifunga mabao nane akiwa ni namba moja kwa utengenezaji wa pasi ndani ya ligi.

Taarifa zimeeleza kiungo huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao wa 2021/22.

Mbali na Chama pia nyota wao Luis Miquissone yupo kwenye hesabu za mwisho kutua nchini Misri kwa ajili ya kujiunga na Klabu ya Al Ahly ya Misri.

Tayari jezi namba 11 ambayo aliyokuwa anavaa Luis amekabidhiwa kiungo mpya Peter Banda ambaye anatajwa kuwa mbadala wa nyota huyo.

Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ambapo Luis hakuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kipo kambini. 

3 COMMENTS:

  1. Simba...
    Viongozi wasifumbie macho idara ya ulinzi kunahitajika kuimarishwa. Suala la Chama pengo Sana lakini hakuna mchezaji anaetarajiwa kudumu muda wote timu moja katika maisha ya soka. Bwalya anaweza kuziba pengo la Chama kwa ufaha zaidi hasa ule uwezo wake wakuwa na Maamuzi ya haraka katika kuchia mipira. Chama alikuwa na hilo tatizo la kuchelewesha pasi za mwisho licha yakuwa kiungo mahiri. Miqisone Kama ataondoka pengo lakini sio pengo la Onyango na ndio maana mashabiki tunalia kuletwa beki kisiki na mwenye uwezo wa kukimbiza ili aje kujenga good partnership na unyango kwa sababu Wawa sio beki mbaya Ila Hana kasi na sio mzuri hata kidoho kwenye mipira ya juu.Uongozi umefanya Jambo la maana Sana kumrejesha Perfect Chikwende. Ni mchezaji mzuri Sana kaliba ya Miqisone au zaidi tatizo hakuwahi kupewa nafasi ya kutosha. Viongozi wangefanya Makosa makubwa Kama wangemtosa Chikwende. Peter Banda ni usajili mzuri Sana. Muhilu,Abdu swamadi,Kibu Denisi na Israeli Mwenda hongera wasaka vipaji wa Simba la msingi hawa vijana wazawa lazima wapewe SoMo la Uraia kwamba kama Kuna wachezaji katika timu hizi wanaotakiwa kuwa na uchungu na kuzipigania kwa jasho lao lote basi nj wao kwanza sio wageni. Lazima wawe na kwanini wao siku ni watu wa kubebwa tu na wageni. Kennedy Juma ni Beck mzuri Sana ila anatakiwa kuwa na ngangari na uharaka zaidi asome kutoka kwa unyango. Kama Bwalya atashuka chini zaidi basi kiungo wa juu apatikane mwenye Kasi na nguvu zaidi. Khasani Dilunga sio winga ni kiungo wa Kati mshambuliaji asilia kwanini anashindwa kumshawishi Mwalimu hata kuiomba nafasi kufanyiwa majaribio hakuna aibu utaendelea kucheza nafasi inayokunyima kuonesha uwezo wako kamili mpaka lini? Vijana wetu wanatakiwa kuchamka au vilabu vyetu hivi vitaendelea kuuza wachezaji wa kigeni kwa Bei Bora kwenda klabu Bora kila msimu wazawa wakiwa watazamaji.

    ReplyDelete
  2. Wabongo wataendelea kusugua benchi na nyie wandishi mtaendelea kuwatukuza wageni

    ReplyDelete
  3. Kaka wajua umenikuna umemaliza umesahau tu kuwasifia mkude Ajib na ndemla kama msimu huu wakituliza vichwa watafanya maajabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic