HARRY Kane nyota wa timu ya Tottenham amewaambia mabosi wake kwamba hayupo tayari kuwa ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao jambo ambalo linamfanya ahitaji kupata changamoto mpya.
Nyota huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya England kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuingia kwenye rada za Manchester City, Chelsea na Arsenal ambao wanahitaji saini yake.
Kwa mujibu wa Sky Sports ripoti zimeeleza kuwa Kane amewaambia mabosi wa timu yake kwamba kwa msimu huu anahitaji kuondoka Spurs jambo ambalo linamfanya afungue njia kwenye timu nyingine ambazo zinamuhitaji.
Mwenyekiti wa Man City, Khaldoon Al Mubarak hivi karibuni alibainisha kwamba wanahitaji kusajili kikosi bora ambacho kitakuwa na ushindani zaidi jambo ambalo linatoa nafasi kwao kuweza kumpata Kane ilikuwa ni baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Tunahitaji kuwa kwenye ushindani na utayari kwa ajili ya msimu ujao. Kwa msimu huu tutaimarisha kikosi kwa kuleta wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa,"
0 COMMENTS:
Post a Comment