August 3, 2021


 KOCHA Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa usajili wa nyota mpya ndani ya kikosi hicho ambaye ni Ben White ulikuwa ni mpango wa mabosi wa timu hiyo.

Nyota huyo ambaye ni beki amejiunga na timu hiyo akitoka Klabu ya Brighton ikiwa ni lengo la kuimarisha ulinzi ndani ya kikosi hicho kinachohiriki Ligi Kuu England.

Ni dau la pauni milioni 50 limetumika kuinasa saini ya nyota huyo na imempa kandarasi ya miaka mitano kudumu ndani ya Arsenal na amepewa jezi namba nne.

Akiwa ndani ya Brighton msimu uliopita beki huyo alipiga jumla ya takolini za uhakika kwa asilimia 53 katika mechi 36 za Ligi Kuu England.

Arteta amesema:"Ben kuja hapa ni mpango wetu wa muda mrefu kwenye kuongeza ulinzi. Ni beki mwenye akili nyingi katika eneo lake akiwa na mpira mguuni," . 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic