MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi leo Jumapili asubuhi alishindwa kujizuia na kujikuta akitokwa na machozi wakati akiwaaga wachezaji, viongozi na mashabiki wa Barcelona, huku tetesi zikieleza kuwa anaelekea PSG.
Akiwa anabubujikwa na machozi katika
mkutano huo Messi amesema: “Maisha yangu yote, bado nahisi sipo tayari kwa hili. Mwaka huu
mimi na familia yangu tulifikia uamuzi wa kusalia hapa licha ya hapo awali
kuleta barua ya kutaka kuondoka.
“Muda tuliokuwa nao hapa umekuwa
bora sana, lakini leo ninalazimika kusema kwaheri kwa haya yote, nimekuwepo
hapa tangu nikiwa na miaka 13, na baada ya miaka 21 naondoka na mke wangu na
vijana wangu watatu.
"Sishawishiki kusema kuwa
sitarejea tena, lakini nashukuru sana kwa kila kitu, kwa
wachezaji wenzangu na ambao nimewahi kucheza nao hapa nawashukuru sana, licha
ya kwamba wengine tulikutana kwa muda mchache.
“Nimekutana na mambo mengi
mazuri, na machache ambayo yalikuwa changamoto kwangu ambayo yalinifanya
nijifunze na kukua zaidi kufikia nilipo sasa, naamini nilijitolea kila kitu kwa
klabu hii na jezi hii kuanzia siku ya kwanza mpaka mwisho.
“Ukweli ni kwamba ninaondoka, licha ya kwamba sikuwahi kufikiri kama kuna siku ningewaaga, ninatamani ningeweza kutamka maneno haya mbele ya mashabiki waliojazana kwenye uwanja huu, lakini kwa bahati mbaya haijawa hivyo."







0 COMMENTS:
Post a Comment